GET /api/v0.1/hansard/entries/595561/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 595561,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595561/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Bw. Spika, pia mimi navaa njuga kukaribisha viongozi wa Kaunti za Kilifi na Vihiga. Ukiona mbari jua zinduna iko nyuma. Hili sio kundi la mwisho kuja kututembelea hapa. Ninawasihi watu wa Kilifi wajisikie nyumbani na wajimwage katika jiji hili. Mimi ni mmoja wenu na pia Seneta maalum. Watu wa Vihiga pia nawakaribisha. Tunaye Sen. Khaniri hapa. Yeye ni kiongozi wa maendeleo kabisa. Kwa hivyo, mjihisi nyumbani na wengine waje pia kwani mikono yetu i wazi kuwalaki. Karibuni."
}