GET /api/v0.1/hansard/entries/595638/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 595638,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595638/?format=api",
    "text_counter": 254,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wamejaribu kutumia boya. Je, yanafanya kazi? Ni wangapi wakirushiwa wana uwezo ya kuogelea? Siwezi kulaumu sana wenzetu ambao walisema kungekuwa na El Nino . Waswahili wanasema kuwa, heri kunyesha ujue panapovuja. Je, tuko tayari? Mswada huu umekuja wakati tunahitaji sana. Tunaomba pia Mwenyezi Mungu atujalie El Nino isitupate kabla hatujajiandaa. Je, ikitokea kwa kaunti moja, kaunti nyingine itatusaidia ama tutangoja mpaka usaidizi utoke Serikali kuu? Ninaunga mkono Mswada huu. Ni lazima tujiandae. Sisi kama wananchi wa Kenya ni kawaida yetu janga likitokea siku mbili ama tatu, tunashughulikia sana lakini katika siku ya nne tunarudi tulipokuwa. Kwa mfano, jambo la dharura likitokea, tunapekuliwa hadi unashangaa kuna nini. Hapa nje ya Bunge kukiwa na jambo la dharura, ndipo utakuta polisi wakirekodi matukio kwenye vitabu, lakini baada ya siku mbili tunarudi kawaida. Ni kama tunachezea janga. Hatuyatii manaani kuwa ni lazima tuwe tayari wakati wowote kwa sababu janga linaweza kutokea na tusingoje mawingu. Dalili ya mvua ni mawingu lakini wakati mwingine tunaweza kukosa. Tusiwe tu tunajihadhari wakati wa El Nino pekee. Kuna mikasa mingi ambayo ikitupata, hatuna uwezo kujizuia. Tsunami ikitokea eneo la Pwani tutashindwa kujisaidia. Kwa hivyo, lazima tuwe tumejiandaa. Mara nyingi Budalangi watu wanaposhawishiwa watoke kwenye sehemu zilizofurika, hawataki kutoka. Tumezoea tukae pale ili tusaidiwe. Tumejidharau hadi tunaona kiwango chetu kwa nchi ni cha nadhifu. Bw. Naibu Spika, nimesema hapo awali kwamba heri kusinyeshe uone panapovuja, lakini saa zingine tunaomba inyeshe ili tujue panapovuja. Je, kabla ya kuvuja, paa letu tumelitengeneza namna gani? Mwisho, ni kwamba lazima tujihadhari kabla ya hatari. Tukiona ambari, tujue zinduna yaja. Siku zote, dudu linalouma tusilipe kidole. Wale wasimamizi wa wa kaunti, pesa zisivujwe. Wakitia mifukoni na wananchi wanatarajia watumie kujinasua kwa mikasa, watu wetu wataangamia na nchi yetu itaangamia pia. Shukran."
}