GET /api/v0.1/hansard/entries/595878/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 595878,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595878/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Spika. Nataka pia kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Kamati ya Kiidara ya Utawala na Usalama wa Kitaifa. Ni dhahiri ya kwamba Meja Mstaafu Shadrack Muiu Mutia amefanya kazi nzuri hapa nchini. Lakini, kama tunavyosema; maisha ya binadamu hubadilika kila siku. Kuna wakati ambao utakuwa mzima na wakati ambao utakuwa na shida na hutaweza kutekeleza majukumu yako. Hakuna aliyetaja kuwa Meja Mstaafu Shadrack Muiu Mutia, hajafanya kazi yake vizuri kwa utendakazi wake. Lakini maisha ya mwanadamu yanazidi kubadilika--- Katika Katiba yetu, Kipengele cha 251, kimetaja uwazi kwamba atakaposhindwa kutekeleza majukumu ya kufanya kazi, hana budi kustaafu. Ninaunga mkono Ripoti hii kwa udhaifu na kuwaomba wenzangu kwa unyenyekefu kwamba tukiangalia Kipengele kile na kazi nzuri Meja Mstaafu Shadrack Muiu alifanya--- Kamishna wa Tume ya Kitaifa ya Kuwaajiri Polisi amefanya kazi nzuri katika utenda kazi wake. Kimaumbile, Meja Mstaafu Shadrack Muiu Mutia hawezi kuendelea kufanya ile kazi sasa hivi. Kamati ilijaribu sana kumtafuta ili aje ajieleze. Lakini Mwenyekiti wa Kamati kwenye masuala kama haya, mkiambiwa mtu ni mgonjwa, ingelikuwa ni vizuri pia kama mngekwenda kumsalimia nyumbani ili mjue ako hali gani na katika hali ya kiutu na kibinadamu, bwana huyu ana tatizo kubwa kiasi gani. Nafikiria hakuna Kanuni za Bunge hili, yaani Standing Orders ambazo zinawaruhusu kwenda mpaka nyumbani kwa mtu kuangalia ni shida gani iliyomfanya bwana au mfanyakazi huyu kukosa kuja hapa Bungeni, katika utenda kazi wake. Hivyo basi, kama wangelipata habari kwamba yuko hospitalini, wangekwenda pale. Kuna umuhimu kwamba Kanuni za Bunge hili zibadilishwe kuwaruhusu Wabunge wanakamati fulani kuwatembelea wafanyakazi kama hawa ili tuwezekujua mbivu na mbichi. Nimemsikia ndugu ya Kiongozi wa Wachache Bungeni, Mhe. Nyenze, akilalamika. Lakini, juu ya kulalamika ni kwamba kazi lazima itendwe na ifanyike vilivyo. Roho yangu ikiwa nzito, ningependa kumwambia kaka yangu, ndugu yangu, kiongoze, Mhe. Nyenze kwamba ni lazima kazi ifanywe hata tukilalamika vipi. Mhe. Spika, tulimpoteza Kamishna Esther Colombini, aliyekuwa mama mchapa kazi. Alivyofariki, mtu mwingine hajapatiwa jukumu la kutenda kazi ile. Amekwenda mbele ya haki-- - Vile vile, ilimbidi dada yetu Naibu Kamishna wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi Bi. Grace Kahindi, kustaafu. Kusema kweli, Tume hii inashindwa kufanya kazi. Hivyo basi, hatuna budi kuunga mkono mapendekezo ya Kamati hii tukiomba kwamba hatuna njia nyingine ila kuhakikisha kuwa majukumu ya kufnaya kazi lazima yatendeke na kazi itendeke. Mhe. Spika, hatuna njia nyingine ila kumwoomba Mhe. Rais aunde tume itakayoangalia matatizo haya na kupendekeza njia ya kumsaidia, na vile vile kumpatia Mkenya mwingine nafasi ya kufanya hii kazi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}