GET /api/v0.1/hansard/entries/595915/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 595915,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595915/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuchangia Hoja hii. Hoja hii inatatiza kidogo kwa sababu Kamishna ambaye tunaongea juu yake ametumikia nchi hii kwa muda mrefu katika nyadhifa mbalimbali. Tumeambiwa kwamba Major Mstaafu Shadrack Mutia, aliletea mabadiliko katika Kikosi cha Utawala. Hadi leo, kikosi hicho kinaendelea vizuri. Tumeambiwa kwamba pia alisaidia kuzima jaribio la mapinduzi ya mwaka wa 1982. Licha ya hayo yote ameyafanya katika nchi ya Kenya, wakati unafika ambapo tunaweka nchi mbele kuliko masilahi ya mtu mmoja. Mhe. Naibu Spika wa Muda, huduma kwa taifa ni lazima. Ukiajiriwa au kupewa cheo katika idara ya taifa, ni lazima upeane huduma kwa sababu ushuru unaotumiaka kukulipa hutoka kwa wananchi ambao wanahitaji huduma kutoka kwako. Mhe. Naibu Spika wa Muda, magonjwa hutokea kwa kila mtu. Ni heri Kamishna huyu astaafu lakini apewe marupurupu yake ili apate matibabu, na pia aishi vizuri. Hii ni kwa sababu amechangia katika ustawi wa taifa hili. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}