GET /api/v0.1/hansard/entries/595916/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 595916,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595916/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Tunaomba Kamati inayohusika kwamba iwapo watamstaafisha Kamishna huyu basi wampatie marupurupu yake kama njia ya heshima kwa vile ametumikia taifa hili kwa muda mrefu na katika nyadhifa mbalimbali. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kama ningekuwa na uwezo ningependa Tume hii ya kuleta mageuzi katika idara ya polisi ifutiliwe mbali. Iwapo umewahi kuwaona makamishna hawa wanapowahoji maafisa wa polisi, utagundua wanatoa vitisho. Vitisho ambavyo wanatoa mbele ya askari wanaohojiwa ni vya kuvunja moyo. Ningeomba Kamati hii itilie mkazo kwa hao Makamishna wanaowahoji askari wasitumie vitisho."
}