GET /api/v0.1/hansard/entries/595917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 595917,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595917/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nakara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2926,
        "legal_name": "John Lodepe Nakara",
        "slug": "john-lodepe-nakara"
    },
    "content": "Kuweka shaka kwa mali ya watu ni jambo ambalo tunaomba Kamati hii iangalie na kuelezea tume hiyo kwamba huwezi kuweka mashaka kwa utajiri wa mtu kwa kuuliza alipotoa mali na kwa nini hatumii pesa zake, na kuuliza mshahara wake ni pesa ngapi. Watu wana njia mbali mbali za kutafuta pesa kama kufanya biashara na kuwekeza mahali fulani. Tume hii imewafuta maafisa kazi bila hatia au kuhusika katika ufisadi. Tunaomba Mhe. Kamama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama na Utawala, aangalie mambo hayo. Hii ni kwa sababu hatutasimamisha huduma ya afisa ambaye amejitolea kuhudumia nchi hii kwa sababu ya kuweka mashaka juu ya mali yake na kuuliza mahali alitoa mali yake. Ningependa kumkumbusha Mwenyekiti wa Kamati hii kwamba, makamishna wanafaa kuwa na huruma, utu na ubinadamu. Unapohudhuria kikao cha hao makamishna wanaoleta mageuzi katika idara ya polisi, unagundua kwamba hawana utu jinsi wanauliza maswali. Wanatumia matamshi makali na kuangalia maafisa na macho makali hata kama afisa alikuwa na mambo ya kuzungumzia anashindwa. Tunaomba Mwenyekiti Kamama awaeleze hawa makamishna wawe na utu kwa sababu hawa maafisa ni watu walio na familia. Nikimalizia, Meja Mstaafu Shadrack Mutia, kwa sababu ya ugonjwa uliompata, tunamuomba kwa heshima ili aendelee kuheshimika akubali kustaafishwa, na aombe tume impatie marupurupu ili aishi maisha mazuri. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}