GET /api/v0.1/hansard/entries/595927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 595927,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595927/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bedzimba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1933,
        "legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
        "slug": "rashid-juma-bedzimba"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Ninakushukuru sana kwani unapokuja ninapata fursa ya kuzungumza. Mara nyingine huwa nabofya mpaka nasinzia. Ninasimama hapa kuunga mkono Kamati ya Usalama wa Taifa kwa Ripoti ambayo imeleta. Ni kweli kwamba inakuwa vigumu kwa vikao vya tume kuendelea kwa sababu ya idadi ya wanachama wao. Ninachukua fursa hii kusema kwamba ndugu yetu Maj. (Rtd.) Shadrack Muiu alikuwa mzalendo aliyejitolea kwa taifa hili. Juzi, tulisherehekea siku ya Mashujaa. Siku zijazo hata yeye atakuja kusherehekewa kama shujaa kwa sababu alijitolea mhanga kwa taifa ambalo lilikuwa linakwenda kwenye mapinduzi. Kwa sasa, inakuwa vigumu kumtaja na tunaangalia wale wa mwanzo. Lakini siku za usoni hata yeye atatambulika kuwa alisimama siku moja kuzuia mapindizu humu nchini. Kwa hivyo ni kweli kikao ni muhimu sana kuendelea, lakini tusivunje heshima yake kwa siku moja. Ningeomba tumpe nafasi aje ajieleze tena, ama wale wanaohusika na matibabu waje watueleze kama kulingana na yale maradhi aliyonayo anaweza kuendelea ama hawezi kuendelea. Kama hawezi kuendelea, tumuondoe kupitia kwa matibabu na alipwe pesa anazofaa kulipwa ili heshima yake iendelee kwa sababu ni mtu ambaye amejitolea kwa taifa hili. Haswa yeye ndiye aliyewatengeneza askari wa utawala. Amejitolea kwa mambo mengi. Ninaiunga mkono Kamati hii lakini huyu Bwana apewe nafasi tupate ripoti kamili. Ikiwa kweli matibabu yake hayawezi kumruhusu kuendelea na shughuli zake, basi astaafishwe. Hata kabla ya kuleta tume, wale wanaohusika na matibabu yake waje watueleze sababu sote hapa kwa sababu hatujawahi kujua yale maradhi anayougua na iwapo anaweza kuendelea na matibabu kwa muda gani. Vile vile, kwa sababu ugonjwa huu aliupata akiwa kazini, inaonyesha kwamba ni mtu ambaye amejitolea. Kama angekuwa mgonjwa akiwa hapa ingekuwa tumesema ni matatizo ya ndani. Lakini huyu alienda kazini na maradhi yakampata akiwa kazini. Kwa hivyo kuna sababu kamili kwamba huyu ni mzalendo. Tusimtoe hivi tu na kumharibia jina. Huyu ni shujaa. Kwa hivyo tumwondoe kishujaa na tumpe heshima zake. Ninakubaliana na Ripoti ya Kamati lakini hilo jambo liangaliwe. Asante, Naibu Spika wa Muda."
}