GET /api/v0.1/hansard/entries/595944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 595944,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595944/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Waliotengeneza Katiba mpya na Wakenya walipoipitisha, tulisema kuwe na Tume ya Kitaifa ya Huduma za Polisi humu nchini kutusaidia katika sehemu ya ulinzi ya serikali. Kwa sababu ambazo zitaongelewa hapa, imekuwa vigumu kwa Komisheni hii kufanya kazi yake inavyostahili. Sababu moja ni kwamba kuna Kamishna ambaye alifariki, pili, kuna huyu mwingine ambaye tunamzungumzia leo ambaye ni Meja Mstaafu Shadrack Mutia Mulu ambaye amekuwa mgonjwa kwa karibu miaka mitatu sasa na hawezi kuhudumu inavyostahili. Mwanzo, ninataka kusema pole sana kwa Meja Mstaafu Mutia kwa sababu ya ugonjwa wake. Hakuna mtu anayemtakia mwingine ugonjwa au maradhi. Hususani magonjwa ambayo yanamweka siku nyingi sana mpaka hawezi kuja kazini na kufanya kazi inavyostahili. Ninaunga mkono Kamati hii na Ripoti walioleta hapa Bungeni kwa sababu inaomba jambo ambalo ni la busara sana. Wanataka hili suala ambalo ni la Kamishna ambaye ni mgonjwa kwa karibu miaka mitatu sasa liende kwa jopo maalum au tribunal . Jopo hilo litaona kama anaweza kustaafishwa au la. Tunaunga mkono kuwa ikiwa jambo hilo litakubalika, apewe marupurupu yake kwa ukamilifu na Serikali imuangalie katika masuala yake ya kutafuta huduma ya kiafya kwa sababu amehudumia nchi hii kwa muda mrefu sana. Ninakubali kwa sababu hatuwezi kuruhusu Tume ya Serikali ikae kwa muda mrefu sana bila kufanya kazi yake. Ile ndoto ya Wakenya na ndoto iliyotunga Katiba kuwa na Tume haifikiwi ikiwa hii Tume haitafanya kazi yake. Vile alivyokataa kustaafu kwa hiari yake, ninakubaliana na Kamati kuwa hili jopo liungwe mkono ili lifanye kazi yake. Ningeomba hili jopo likikaa, lisicheleweshe hii ripoti kwa sababu litakuwa limemtia hofu na wasiwasi Maj. Shadrack kwa kutojua mwelekeo. Nchi inashindwa kusonga mbele katika hii sekta kwa sababu ya masuala ambayo yanaweza kuangaziwa."
}