GET /api/v0.1/hansard/entries/595953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 595953,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/595953/?format=api",
"text_counter": 283,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Tume hii inawatatiza watu wengi. Ninashukuru Kamati ya Masuala ya Usalama na Utawala. Kuna mambo yanaendelea kwa wafanyikazi wa Serikali ambao ni polisi. Kama juzi tuliona mengi kwa gazeti. Maafisa wa Serikali walisimamishwa na wengine 70 walifutwa. Ingekuwa muhimu pia kuangalia kwa undani kwa sababu ukiambiwa watu 70 wamefutwa kazi ama wameondoka, sijui kama wote ni wabaya ama wote wataenda na malipo yao ya uzeeni ama wataenda kwa njia gani. Kwa hivyo, ninaunga mkono Kamati ya Masuala ya Usalama na Utawala. Waendelee kuangalia hayo mambo kwa sababu tukizungumzia kustaafu kwa Maj. (Rtd.) Muiu, pengine kesho utapata kesi nyingine. Kamati ya Masuala ya Usalama na utawala inafaa kuangalia kindani ni nini kinachoendelea kwa sababu ukiangalia hata saa hii, utapata tunayo shida kupigana na utovu wa usalama. Hujui kama ni kwa sababu ya haya mambo yote wanafanyiwa yanamfanya ashindwe kufanya kazi au ni mambo mengine. Pengine hajui atatoka kesho na atatokaje. Ninaunga mkono hii Ripoti ya Kamati lakini ni vizuri waangalie idara ya polisi. Tuna shida kubwa katika idara ya polisi. Jambo hili linapaswa kuangaliwa kwa kina."
}