GET /api/v0.1/hansard/entries/596192/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 596192,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/596192/?format=api",
    "text_counter": 221,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nakara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2926,
        "legal_name": "John Lodepe Nakara",
        "slug": "john-lodepe-nakara"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii wakati ambapo Bunge linaenda kwenye mapumziko. Ni wakati wa kwenda kuelimisha umma juu ya sheria ambazo tumezitengeneza hapa, kwa maana wengi wao hawajui kusoma na hawajahi kusikia kuhusu sheria hizo. Ni wakati pia ambapo Wabunge wataenda kuwaelimisha ili wajue jinsi ambavyo sheria hizo zitawasaidia na kuongoza maisha yao ya kila siku. Pia tutasikia maoni ambayo wangependa yahusishwe kwenye sheria ambazo tutatengeneza baadaye. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni wakati pia wa kwenda kuangalia miradi ambayo imejengwa kwa kutumia pesa za ustawi wa maeneo Bunge katika maeneo yetu. Itakuwa ni wakati wa kufungua miradi hii na kuipeana kwa wananchi, ili wafurahie matunda ya pesa za ustawi wa maeneo Bunge; hii ni njia moja ya kupanua maendeleo katika nchi hii. Pia, huu ni wakati mwema wa kuendelea na maombi kama Jubilee juu ya ndugu zetu wawili, Naibu wa Rais, Mhe. Ruto na Arap Sang, ambao kesi zao ziko kule ICC. Tutaendelea kuwaombea na kuwaweka katika mkono wa Mungu ili majaji watakapofanya uamuzi wao, waufanye kwa njia ya busara bila kupendelea au kufuata siasa. Tunataka kwenda kupumzika ili tuje baadaye tukiwa tumechangamuka na tuna nguvu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}