GET /api/v0.1/hansard/entries/596418/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 596418,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/596418/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mositet",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 608,
"legal_name": "Peter Korinko Mositet",
"slug": "peter-korinko-mositet"
},
"content": "Asante sana, Bw. Mwenyekiti. Mimi si wakili lakini kulingana na yale Maseneta waliotangulia wamesema, Spika alitoa mwelekeo wake jana lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kuukosoa kwani Maseneta hawakupewa fursa ya kuukosoa mapema kabla ya kikao hiki. Tunajua kwamba kulikuwapo na Kamati ya Uwiyano iliyokaa chini na kuzungumza lakini hawakukubaliana. Jana, Bw. Spika alitoa mwelekeo lakini tutakayoizungumzia sasa ni ripoti ya Kamati ya Uwiyano ambayo haijaakifishwa mbele ya Seneti. Kusema ukweli Rais wetu anapewa aibu. Bw. Mwenyekiti, naomba tuihairishe Hoja hii ili Bunge la Seneti lisije likapata aibu. Ni kama tuko kwa majaribio. Kwa hivyo, nakusihi utumie hekima yako kuhairisha mjadala huu hadi tukae chini tutatue tashwishi zilizopo. Hoja hii haikuletwa kama ripoti kwa Seneti."
}