GET /api/v0.1/hansard/entries/59642/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 59642,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/59642/?format=api",
    "text_counter": 335,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Mda. Ninaomba nichukue nafasi hii kuiunga mkono Hotuba ya mheshimiwa Rais na kuangazia masuala mawili au matatu ambayo hayakuangaziwa kwenye Hotuba hiyo. Kwanza, nitazungumzia Mpango wa KKV. Kama tunavyojua, mpango huu haujawanufaisha vijana, na tunaiomba Serikali ifikirie njia nyingine tutakayotumia kuwasaidia vijaana wetu. Pili, nitazungumzia suala la ubinafsishaji wa Bandari ya Mombasa. Ninashukuru kwamba Waziri wa Uchukuzi yuko hapa. Tunasema kwamba miundo msingi kwenye bandari hiyo iboreshwe lakini bandari iendelee kuhudumia watu vile ilivyo. Rais hakulizungumzia suala la ubinafsishaji wa Bandari ya Mombasa kwenye Hotuba lakini nimetumwa na watu wa Pwani nije hapa kusema kwamba ubinafsishaji wa Bandari ya Mombasa hauhitajiki. Tunachohitaji ni kuboreshwa kwa bandari hiyo. Tatu, nitazungumzia madini. Katika Mkoa wa Pwani, na hata kwenye sehemu ninayowakilisha hapa ya Wundanyi, kuna madini mengi. Tungependa kuona shughuli katika sekta hii, ili iboreshwe. Tungependa kubuniwe viwanda vitakavyowezesha kutumiwa kwa madini hayo humu nchini ili kuongeza kazi kwa vijana. Bw. Naibu Spika wa Mda, hatupati faida yoyote kutokana na kuweko kwa wanyamapori, kama watu wa Taita Taveta. Tunaomba jambo hili litiliwe maanani. Ninashang’aa ni kwa nini Rais aliliacha jambo hili, nje ya Hotuba yake. Mwisho, nitazungumzia suala la maji kutoka Mzima Springs. Mpaka sasa, tungali tunayalilia maji kutoka Mzima Springs. Ijapokuwa Rais hakulitaja jambo hili kwenye Hotuba yake, tunatarajia kwamba maji yatatoka Mzima Springs yaende Kishushe, Mwakitau na Mwatate, halafu yashike njia kupitia Voi, na kwenda Mombasa. Ni jambo la kushangaza kwamba sisi Wataita, hatufaidiki na maji kutoka Mzima Springs wakati wenzetu wa Mombasa wananufaika nayo. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hotuba ya Rais."
}