GET /api/v0.1/hansard/entries/596585/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 596585,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/596585/?format=api",
    "text_counter": 384,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii, ili nami niunge mkono Hoja hii ya Sen. Kittony. Hoja hii imebobea kama mamangu, Zippora kwa sababu ni Hoja ya maana sana ambayo imechukua muda mrefu, na tujuavyo wakati ni mali. Lakini sisi hatuoni kama wakati ni mali kwa sababu muda mwingi sana tunaharibu brarabarani, muda mwingi sana hatujui tutafika salama ama vipi kwa sababu ukiangalia ule msongamano, haujui nani atakuzaba kofi au atakupiga risasi. Tulitembelea Uchina, na tulishangazwa kuona kuwa sera zao zinahimiza kila familia kuwa na mtoto mmoja. Tulijiuliza mbona hii nchi haina watu, ilhali tunasikia kwamba wamezaana sana. Tulishtuka sana tulipofika chini kuingia kwenye gari moshi zao, tuliukuta umati ambao hata hatujauona maishani, watu wengi sana. Lakini, jinsi Wakenya tulivyo, kila mtu anataka kuonekana kwamba ana gari. Magari yote lazima yaingie Mjini na pengine jamii moja ina magari matano; zote zinakuja kazini. Tukiangalia pia tunaona kwamba nidhamu imechangia sana. Unapoagangalia barabara, hazina nafasi. Hata barabara zikipanuliwa, bado msongamaono ni ule ule. Tufanye aje? Ukiona akina mama wamejifunga kibwebwe kama Sen. Kittonyi, ujue kwamba kuna mchezo, mbao anataka kucheza. Hoja hii ina maufaa sana. Msongamanao huu unasababisha vifo kwa sababu ambulensi ikitokea hujui mgonjwa yuko mahututi kiasi gani. Wagonjwa wengi hupoteza uhai barabarani. Muda pia hupotezwa. Hakuna anayetamani awe mgonjwa na apitishwe kwa barabara yenye msongamano wa magari. Kaunti nyingi zimenunua ambulensi, na kwa hivyo, barabarani ni kelele ishara ya mgonjwa mahututi. Lakini kwa sababu ya msongamano wa magari, hatapishwa. Hoja hii itasaidia wagonjwa wasife njiani bila kufikishwa hospitalini. Msongamano barabarani huchelewesha wagonjwa na wanaweza wakaishiwa na hewa kwenye vifaa vya usaidizi. Madam Spika wa Muda, kuna siku tumekaa barabarani hadi alfajiri. Ni kilomita chache lakini kulikuwa kunanyesha na pia msongamano wa magari. Ukifika nyumbani, una saa mbili pekee ya kulala. Wakati mwingi tuko barabarani hadi watoto wamesahau sura zetu kwa vile tukitoka alfajiri, tunarudi saa nne usiku. Tumepoteza muda mwingi kwa kusafiri barabarani. Wakati mwingine unatamani kutembea kwa mguu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}