GET /api/v0.1/hansard/entries/596587/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 596587,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/596587/?format=api",
"text_counter": 386,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Msongamano huu umetutesa sana. Kuna madereva ambao wana ugonjwa wa kisukari au wa high blood pressure na wanaweza kufia njiani. Ni bugdha ilioje ambayo imetukiri? Lazima tuone wenzetu wanafanya namna gani. Tunapoondoka nchi za nje kusoma, lazima turudi na tuige wenzetu ambao wameendelea. Huu msongamano tutasuluhisha namna gani? Agunduaye nywele ndio mganga. Leo Sen. Kittony anataka tugundue zile nywele ili tusaidike kama Wakenya na tuwe kama nchi zingine. Tusipozingatia muda kwenye harakati zetu za kawaida, tutapata shida. Pia kama Wakenya, tuko na tabia ambayo sisi sote tunajipata barabarani kwa wakati mmoja. Kuna uwezekano kuwa tunawacha koti kazini na kutoka nje kwa ziara zetu ndiposa tunasababisha msongamano. Je, hili jinamizi tutalitibu vipi? Tukilitibu, tutapata manufaa kubwa na hata uchumi wetu utapanda. Wale walaghai ambao wanachelewa kazini watagunduliwa. `Mswada huu umekuja wakati mwafaka. Sisi Wakenya lazima tuwe na nidhamu tukingoja barabara au reli zitengenezwe. Ni kawaida yetu tukikosa, hatuna haja kuwaambia wenzetu samahani. Hatuwezi kuwalaumu kwa vile labda mtu ana mgonjwa ndani ya gari ama anasafiri kwa ndege na anachelewa. Siku moja nilikuwa Likoni Ferry na kulikuwa na msongamano mkubwa lakini nilipita magari yote. Nilipofika mbele, nilipatana na polisi. Nilimdanganya kuwa tumbo linaniuma na kwamba naenda chooni. Tumekuwa waongo kwa sababu ya jam. Pale Likoni ferry watu wanakanyagana kila wakati. Si msongamano wa magari pekee, pia msongamano wa watu kwenye Likoni ferry kila wakati. Ukivuka kivuko cha ferry saa sita usiku, Ferry itakaa upande ule saa moja na irudi upande huu saa moja. Kwa huo wakati, utakuwa umelala na badala ukanyage breki, ukakanyaga acceleration na uingie kwa maji. Kuna kesi kama hizo. Hizi barabara zetu zinatufanya tuwe wanyonge, tupoteze uhai mapema na pia tupoteze biashara zetu. Saa zingine mtu anatamani afike kwake mapema na inabidi atoroke mapema. Barabara hizi zinatufanya tukose maono na tubaki tukitatizika. Naunga mkono Hoja hii. Asante."
}