GET /api/v0.1/hansard/entries/597490/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 597490,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/597490/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nampa pongezi tena ndugu Sen. (Prof.) Anyang'-Nyong'o kwa sababu tumezoea kupongeza watu ambao ni maiti au mamati. Saa hii mtu akifungua runinga, atauliza ni nani amekufa kwa sababu hatupeani sifa mpaka mtu awe amekufa. Hii ni Hoja nzuri kwa sababu twapeana sisi wenyewe heko; tutakuwa mashujaa. Shujaa ni nani? Shujaa sio lazima apigane. Huyu Sen. Kipchumba pia ni shujaa kwa sababu ya ushujaa alioufanya. Bwana Spika wa Muda, sio rahisi mtu awe kilema ili aweze kusema ni vipi alipata ulemavu huo. Mbarika hii imekuwa muhimu sana. Utaona ya kwamba bado itikadi zetu zinatuvuta nyuma. Watu wengi bado hawataki kukubali kwamba ugonjwa huu wa polio unaweza ukazuilika. Ukiangalia, yamesemwa mengi na Sen. (Dkt.) Khalwale. Mama mja mzito lazima apate chanjo ambayo itamsaidia. Mama anapojifungua, yule mtoto lazima apate chanjo zote. Unapodungwa na msumari, lazima pia uangalie matibabu yake ni gani. Serikali inafaa kutoa huduma hii pasipo kuwalipiza waathiriwa. Bwana Spika wa Muda, kama Wakenya tumezoea kusifiana kama mtu amekufa. Ninataka kutokea leo tubadilike na tupeane sifa kochokocho kwa kila mtu ambaye anatenda mambo ya maana katika nchi yetu. Sio rahisi kwa wagonjwa wa kupooza kutoke nje. Kule kwetu, kuna watoto ambao hawajatoka hata nje. Sen. Kipchumba alijitokeza kinagaubaga na akasema kwamba alikuwa ameathiriwa na ugonjwa wa kupooza. Pili, amesema kwamba tusijifiche watoto kwa nyumba kwa sababu ya ulemavu. Watoto wetu wengi wanafichwa kwa nyumba mpaka siku ya kufa kwao. Imekuwa ni aibu mtu kusema kuwa ana mtoto ambaye amelemaa. Kwa hivyo, utaona hii mbarika Kipchumba ameipasua sio mbarika rahisi kwa sababu amekuwa kielelezo, amekuwa mfano, amekuwa ni mtu ambaye anaeleza watu kwamba, hata kama umelemaa, maisha yanaweza kuendelea na yakawa mazuri kuliko vile yalivyokuwa. Bwana Spika wa Muda, wengi wetu tumekuwa na huzuni sana kutoka aondoke kwa sababu kama hapo awali, nilivyosema ni kakaangu. Tulishindwa hata kujua tutamwambia jambo gani kwa sababu alikuwa ni mmoja wetu, kaka yetu na rafiki yetu katika Bunge hili la Seneti. Lakini leo, tunaona kwamba Mwenyezi Mungu amempa hadhi nyingine. Kama tunavyosema, mlango huu ukifungwa, Mwenyezi Mungu atakufungulia mlango mwingine. Kwa hivyo, tunataka kumpa hongera kabisa kwa sababu kama ni mtu mwingine, tungesikia labda alijinyonga, tungesikia labda na yeye pia hatoki nje, lakini ametuonyesha mfano ambao watu wengi sana isingekuwa jambo rahisi kutoka na kuonekana tena kwenye runinga na kuwaelimisha wengine. Pia, si rahisi mtu mwingine kusema, usikanyage hapo pana msumari umenidunga. Wengi wetu tungenyamaza mwingine naye adungwe ili tumwambie pole. Kwa hivyo, ana roho ambayo watu wengi hawana. Ninataka kuwaomba wale walemavu wote waige mfano wa Harrold Kipchumba wajitokeze ili tuishi kama Wakenya, ili nao pia watachukuliwa kama binadamu wale wengine. Bwana Spika wa Muda, twahitaji utafiti zaidi kwa mahabara yetu ili kumaliza magonjwa kama ugonjwa wa polio ama kupooza. Tuangalie vifaa vyetu vyahifadhiwa vipi, kwa sababu tukiangalia zile chanjo, lazima ziwe zinahifadhiwa vizuri. Tumenunua ambulansi, je, tuna friji za kuhifadhi madawa hayo? Lazima tuangalie vitu ambavyo ni The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}