GET /api/v0.1/hansard/entries/597492/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 597492,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/597492/?format=api",
    "text_counter": 305,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "muhimu zaidi. Tukiangalia friji tunaweza kusema ni chombo ambacho hakina maana. Kwa hivyo, labda tutaangalia ambulansi tu. Sasa lazima tuangalie vitu gani vidogo vidogo pale kwenye mahabara yetu ni muhimu zaidi na vitatusaidia zaidi. Lazima ugonjwa wa kupooza uwe ni ugonjwa ambao tutauchukulia kama umepitwa na wakati. Bwana Spika wa Muda, tulikuwa kule Geneva kwenye mambo ya ulimwengu mzima kuangalia mambo ya hospitali, magonjwa na maradhi. Kuna nchi ambazo tayari zimekabiliana na ugonjwa huu wa kupooza na lazima tuwe tutaangalia mama mjamzito anapojifungua anahitaji kusaidiwa vipi. Isiwe kwamba mtoto anapooza kwa sababu ya magonjwa ambayo tunaweza kuzuia kama vile ugonjwa wa kupooza. Tunajua kwamba kuna ya Mwenyezi Mungu, lakini mpaka iwe ni ajali ambayo imebidi tulala, tutakuwa walemavu lakini tusilemae kwa sababu ya polio. Tusilemae kwa sababu ya magonjwa ambayo tunaweza kuyazuia. Lazima tutahadhari kabla ya hatari. Mara nyingi utaona sisi kila siku twapelekana – Waingereza wenyewe wanasema “ postmortem ”. Haifai na tutakataa postmortem. Tunataka kila kitu kiwe kitafuata na kuenda vile inavyohitajiwa na hatutauona tena huu ugonjwa wa polio katika nchi yetu, isipokuwa kwa wale ambao tayari wamekomaa sana. Bwana Spika wa Muda, twataka kila mzazi ambaye ana ugonjwa ule, na kila mzazi ambaye hakupata, awe anafanya bidii ili waasithiriwe na polio. Nimesema hapo awali tunataka utafiti zaidi kwa sababu tukiangalia kama kile kisa ambacho kilitokea kule upande wa Magharibi, watoto ambao walilemaa kutokana na chanjo ambayo walipewa, lazima tuwe waangalifu kama wauguzi, mimi nikiwa mmoja wao. Ni lazima tujiulize; je, ule ulemavu umetokana na ile chanjo? Je, ule ulemavu umetokana na mtu kutojua ni dawa gani atatumia kuwatibu wagonjwa wake? Je, ile chanjo iliwekwa mahali ambapo panafaa? Tumesikia mifano ambayo imetolewa na wenzangu ambao wamenitangulia, Lazima tuangalie kwa sababu hivyo ni vitu vidogo lakini vinaweza kuharibu maisha ya mtu. Ni kitu ambacho kinaweza kumfanya mtu afikirie kwamba hafanani na wengine. Ulemavu sio jambo rahisi kwa sababu utakuwa mgonjwa na wale wengine wataendelea na shughuli zao za kila siku. Utakuwa mgonjwa, lakini wenzako watacheza mpira na wewe huwezi kwa sababu mama hakukupeleka kwa wakati mwafaka kupata matibu dhidi ya polio. Kwa hivyo, huu wote ni uangalifu. Nimesema tuwe waangalifu; mama akiwa mjamzito, tunataka pia kina baba wawe pale. Tukiwa wajawazito tubembelezwe ili tuende kwa hospitali kupata chanjo. Ninamwona Seneta Kanainza anapiga makofi. Ningetaka kumwambia kwamba ni lazima ubembelezwe na ukumbushwe kwa sababu huo ndio wakati ambapo twataka kukumbushwa. Tunataka kubembelezwa na kubebewa vipochi ambavyo havina pesa; ambavyo viko tumboni. Msingoje vipochi ambavyo vina pesa. Bwana Spika wa Muda, utaona mama lazima alindwe. Tusaidieni kama kina mama. Tutafanyaje kupunguza ulemavu huu? Tunapoenda kujifungua, tunaomba wanaume pia wakae nasi pale. Kiuno muwe mtatuangalia na sisi pia. Msitungojee tu nyumbani. Ukiangalia ulemavu huu, utagundua kwamba ugonjwa huu unaletwa na mambo mengi sana ambayo yanaweza kuzuiliwa. Kama nilivyosema hapo awali, lazima tujihathari kabla ya hatari, na unaona vile hatari ni nyingi. Pia, tuwe waangalifu barabarani. Sio polio tu ambayo inaleta ule ulemavu. Kama tunavyosema, “hujafa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}