GET /api/v0.1/hansard/entries/597494/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 597494,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/597494/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "haujaumbika” na chochote chaweza kutokea mpaka ushangae kama kweli huyu ni mimi, Sen. Mvita. Wakati huo umejikunja na kurudi mdogo kama futi mbili. Sio jambo jema. Lazima tuangalie ni vitu gani, yule mtu mwingine anajipenda na ana uhai kama ulivyopewa wewe. Hakuna mmoja wetu ambaye ana nguvu ama anatakiwa na Mwenyezi Mungu kufupisha uhai wa mwenzake. Bwana Spika wa Muda, jambo la tisa ni kwamba lazima tuwe waangalifu, lazima tupendane, lazima tutaangalia kama tunavyo vile vifaa, lazima kuwe na wauguzi mle hospitalini, lazima kama hivi sasa tumeenda kwenye mambo ya ugatuzi, hospitali zetu zahitaji nini? Kuna vitu vidogo kama friji ama jakuuzi ambavyo hatuna. Jambo la muhimu sana kwenye mambo ya polio ni kama tutaangalia ulemavu. Inafaa tuangalie kwamba zile chanjo zetu tumezinunua wapi? Je, tuwe waangalifu ili tujue tarehe ya chanjo hiyo ipo sawa. Hapo awali, mtu anatoa tu kwenye friji na anadunga. Mbona hajidungi yeye mwenyewe kama ni sawa? Lazima tupendane na tuwe waangalifu zaidi. Shukrani, naunga mkono Hoja hii."
}