GET /api/v0.1/hansard/entries/598336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 598336,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/598336/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Nikichangia Hoja hii, nitaangalia mambo mawili. Kwanza, hata kabla tuzungumze kuhusu kuleta mafunzo kwa wale wahudumu ambao wanastahili kututibu katika hospitali zetu, ni lazima tuangalie ikiwa hospitali zetu ziko na vile vifaa ambavyo vinahitajika. Baadhi ya masuala ambayo yanatokezea kwa dharura mashambani, utapata kwamba baadhii ya zile hospitali ambazo ziko kule hazina vifaa ambavyo vinastahili, na ambavyo vinaweza kushughulikia masuala ya dharura. Ndio maana wakati mtu anapoumia, wakati ambao hali za kighafla zinatokea, vile wanavyopelekwa ni rahisi kupoteza maisha yao."
}