GET /api/v0.1/hansard/entries/598337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 598337,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/598337/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Nitatoa mfano katika eneo langu la Kaloleni na eneo lile jirani la Rabai. Unakuta wakaazi wa sehemu hizi wanategemea sana ule mti wa mnazi. Wengi wale ambao ni wajuzi wa masuala ya kugema, hasa ile pombe ya mnazi, kuna wagema wengi sana ambao kila siku wanapoteza maisha yao kwa sababu ya kuanguka kutoka miti hiyo ya minazi. Hata kabla ya masuala ya bodaboda na magari kutokezea, miti ya minazi imekuwa ni baadhi ya sababu ambazo zimeacha watu wengi wamepoteza maisha yao. Lakini kinachostaajabisha katika sehemu hizi ni kwamba hospitali zake bado ziko chini. Ikiwa hatutakuwa na vifaa ambavyo vinastahili, basi kila siku tutapoteza watu wetu."
}