GET /api/v0.1/hansard/entries/598338/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 598338,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/598338/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Ni kweli kama vile Hoja inavyosema kwamba wengi ambao wataenda kwa hospitali hizo kuhudumiwa kwa mara ya kwanza wanapata watu ambao sio wataalamu katika taaluma hiyo. Ikiwa mtu amekuwa mgonjwa, kwa mfano, amepata ajali na afike apate mtu ambaye si mtaalamu kwa suala fulani, ni rahisi kwa mtu huyu kupoteza maisha yake. Ndio maana ningependa kuunga mkono kwamba kuna haja kweli ya kuhakikisha ya kwamba mafunzo maalumu ya afya ya watu wetu itafanyika hasa kwa madaktari na hata watu wengine ambao wanaweza kutusaidia kwa mambo kama hayo. Mambo haya yakifanyika, naamini yatasaidia watu wetu na tutaokoa maisha ya binadamu."
}