GET /api/v0.1/hansard/entries/598377/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 598377,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/598377/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Ningetaka kumshukuru Mama wa Taifa, Margaret Kenyatta, kwa sababu amejaribu kufikia akina mama walio hata ndani sana ndio wasaidike wakijifungua na wanapokuwa na magonjwa mengine. Watakaofundishwa kuwasaidia watu wetu, wanafaa wawe wamejitolea. Mgonjwa hawezi chochote. Wengine wanapata shida sana na wanahitaji kuangaliwa zaidi na kushikiliwa. Kwanza, ujuzi si ile nguo ambayo umevaa. Tumekuwa na wengi ambao wamejifanya kama wamefundishwa na kupata huo ujuzi lakini kumbe wamenunua koti nyeupe na kila wakipita, haujui kama ni wauzaji wa nyama au ni daktari. Tunawaita madaktari kwa sababu ya nguo. Ukiangalia hospitali ambazo ziko katika maeneo yetu, utapata kuwa ni watu ambao wameweka biashara na hawana haja na watu. Wakati kama huu wa mvua ya mafuriko, watu wengi wanazama kwa sababu hakuna mtu ambaye anaweza kuwatoa kwa maji. Ule ujuzi haupo. Kwa hivyo, tukiwa na huo ujuzi, mambo kama hayo hayatatokea. Wakati nyumba moja ilianguka kule Nyamakima ambayo ilikuwa inaitwa “Kihonge”, tulingojea siku nzima au mbili ndio wageni waje wawatoe watu chini ya mawe. Kama watu wetu wengekuwa na ujuzi, tungeweza kuwaokoa watu wengine. Watu hawa walipoteza maisha yao kwa sababu hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na ujuzi wa kuwatoa chini ya mawe. Wakati tunaongea kuhusu hospitali zetu, tunajua kwamba kuna shida nyingi. Tumewafundisha watu lakini hatuna vifaa vya kutosha. Kwa mfano, katika ile kesi ya mama katika Hospitali ya Kiambu, hatujui shida ilikuwa wapi. Labda shida iko upande wa yule ambaye alikuwa anunue mafuta au kwa daktari. Hatujajua. Hata tukijua shida ilikuwa kwa nani, mama ameshaaga dunia. Kwa hivyo, tunahitajika kuangalia mambo haya haswa wakati huu ambao tunashughulikia mambo ya afya. Ninaunga mkono Hoja hii. Tuendelee kuwashikilia watu wetu wote, haswa kwa mambo ya afya. Ukiwa na afya njema, wewe ni tajiri. Nikimalizia, ningetaka kuwaambia Wabunge wenzangu kuwa wamesalimiwa na watu wa Ruiru. Wameniambia kuwa Wabunge wanafanya kazi nzuri na waendelee kushikilia Serikali ya Jubilee. Asanteni sana."
}