GET /api/v0.1/hansard/entries/599525/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 599525,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599525/?format=api",
"text_counter": 312,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bi Spika wa Muda, ninaunga mkono Mswada huu. Mwaka wa 2004, kabla sijaingia Bunge, nakumbuka vizuri nikisoma na kusikiliza vyombo vya habari vikisema kwamba Mswada wa kuwapa watoto wa maskini na hasa wale ambao hawajapata stakabadhi zao nafasi ya kuzipata umepitishwa Bungeni kwa juhudi zake Sen. Musila. Mwaka wa 2008, niliingia Bungeni na Sen. Musila akiwa Mbunge wa Mwingi alilifufua jambo hili na likazungumziwa mara ya pili. Katika Seneti hii sasa, jambo hili limekuja hapa, limezungumziwa, limepitishwa na leo tunalijadili jambo hilo tu. Swali ni; je, ni nani ambaye hafanyi kazi yake katika taifa letu? Hatufai kuzungumza sana juu ya Mswada huu kwa sababu ni dhahiri kwamba jambo tunalolizungumzia na kulisisitiza linawahusu watoto wa maskini. Hakuna mtoto wa mtu anayejiweza ambaye hajachukua stakabadhi zake katika shule yoyote ya upili. Lakini wale watoto wa maskini ndio tunaowazungumzia. Leo ninataka kusema kwamba Sen. Musila labda katika mijadala na miswada iliyopita The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}