GET /api/v0.1/hansard/entries/599527/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 599527,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599527/?format=api",
"text_counter": 314,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "mbeleni, Bunge zote hazikuwa zimeweka mikakati ya hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa kama mtu hatafanya aliloagizwa kufanya. Lakini kwa sasa, tunaona kwamba kama Mwalimu au mtu yeyote atavunja sheria hii, atatozwa faini isiyo chini ya Kshs800,000 au kifungo kisichopungua mwaka mmoja. Labda mikakati hii itafanya kazi. Lakini swali ni; je, katika nchi yetu ya Kenya, kwani ni lazima kila kitu tutumie shingo ili tuende mbele? Lazima kupinda sheria na kulazimisha watu kufanya kazi ambayo wanastahili kufanya kama majukumu yao, watoto wa taifa hili na watu ambao wanajali maslahi ya nchi hii? Bi. Spika wa Muda, tukiwa katika hali hiyo, utagundua kwamba mwalimu katika shule fulani anaweka stakabadhi za watoto waliomaliza shule mwaka wa 1990, 1991, 1995, 1998 au 2000. Mtoto akijaribu kwenda kuchukua stakabadhi yake, anaambiwa alipe karo ambayo ni malimbikizi ya miaka nenda,miaka rudi. Katika shule ambayo nimefanya harambee na kusikiza matatizo yao, kila mwaka kuna bajeti ya shule ambayo inakisiwa kutayarishwa. Lakini haihusu malimbikizo hayo ya karo ambayo haijalipwa. Dhahiri ni lazima kwamba huyu mtoto akienda kuchukua stabakadhi yake, aende na pesa ili aipate. Swali ni; je, hii pesa inatumiwa kumlipa nani? Tunapigania maslahi ya walimu sana. Wengine wetu tuko kortini leo kwa sababu ya kupigania maslahi ya walimu. Tunataka kuona elimu katika taifa letu ikikuzwa hasa kwa wasiojiweza na ndiyo sababu tunasema kwamba badala ya kupata pesa ya kulipa walimu, Ksh25,000 au Kshs30,000 kwa kila mwalimu kwa kila mwezi, pesa hizo tunazitumia kununua kalamu moja ya wino kwa Ksh8,700 ilhali nchi hii ya Kenya haiwezi kumsaidia mtoto wa maskini kupata stakabadhi zake. Serikali hiyo hiyo inanunua kipande cha sabuni ya panga kwa Kshs37,500 bila aibu. Na tukizungumzia mambo kama tunavyozungumza leo, watasema; “weka huyo ndani.” Bi. Spika wa Muda, ni dhahiri kwamba kutoka tupate Uhuru wetu, hakuna kiongozi ambaye amewafikiria wasiojiweza. Mtu ambaye nimesikia akijitokeza wazi bila kuficha na kusema kwamba ni mtetezi wa wanyonge ni Sen. (Dr.) Khalwale."
}