GET /api/v0.1/hansard/entries/599529/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 599529,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599529/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Lakini walioweza kukalia madaraka ni zulia nyekundu, mkeka mwekundu na magari 20 barabarani. Ni mambo ambayo ukichukua gharama ya mtu mmoja kwa siku moja inawakandamiza watu 100,000. Halafu tunasema kwamba tuna taifa letu ambalo tunaweza kujivunia lakini mimi nasema kwamba nchi yetu imekuwa ni nchi ya kuvumilia, sio nchi ya kujivunia kwa sababu asiyejiweza bado yuko chini. Bi. Spika wa Muda, ninashangaa ni kwa nini hatuyaoni mambo haya? Mpaka leo Wakenya ambao tunajidai kuwa watu wanaojiweza, tunaishi kama mahabusu. Kenya ni nchi ya kipekee ambayo unapata mtu anakaa kwa nyumba yake na kwa mlango, kumewekwa mlango wa chuma na kufuli mbili, tatu au zaidi. Juu ya hayo kuna askari. Nyumba anayolala mwenyewe imewekwa chuma kila pembe hadi dirishani. Hiyo nyumba ikipata moto, ni kufa tu. Hata wa kumwokoa hana pahali pa kupitia kwa sababu hakuna muda wa kuvunja vile vyuma na kutoka. Sisi tungelikuwa ni watu wa kujali, hatungekuwa tunalizungumzia jambo hili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}