GET /api/v0.1/hansard/entries/599531/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 599531,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599531/?format=api",
    "text_counter": 318,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Watu wamefika kwa nyumba ya Sen. Musila, pia wamefika kwangu na kwa kila Seneta hapa. Hakuna Seneta yeyote hapa anayeweza kusema kwamba hajaamka asubuhi na kukutana na msongamano wa watoto na wazazi wao. Wakija kusema kwamba, kwa mfano, kazi ya polisi au jeshi inakuja, nisaidie Mheshimiwa niende kwa shule nichukue stakabadhi za mtoto wangu ambaye alimaliza shule miaka mitatu iliyopita ili aweze kuajiriwa kazi ile ya jeshi. Bi. Spika wa Muda, ukitazama, watu wanaofika sio chini ya ishirini na kila mmoja anadaiwa kati ya Kshs30,000 na Kshs40,000. Hakuna Seneta ambaye anaweza kupata pesa hizo kila mwezi ili atoe. Inatoka kwa Serikali na ni lazima Serikali ifanye kazi hiyo. Tukipitisha Mswada huu, ninataka kuona kwa mara ya kwanza, Rais wa nchi hii akiweka sahihi na kutoa amri kwamba ameweka sahihi yake na ni lazima hii itimizwe ili watoto wa maskini wapate stakabadhi ili waweze kujimudu. Bi. Spika wa Muda, hakuna mtu anaweza kukuajiriwa leo, hata kama ni kufanya kazi ya chura bila kuulizwa vyeti vya shule. Wale watoto hawana, ilhali sisi tunakuja hapa, tunazungumuza---"
}