GET /api/v0.1/hansard/entries/599533/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 599533,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599533/?format=api",
"text_counter": 320,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bi Spika wa Muda, kazi ya chura ni kazi ya kusafisha vyoo. Tunaibatiza isiwe chafu sana. Hiyo ndio kazi ya chini sana ambayo mtu anaweza kuuliza, lakini bila kuwa na stakabadhi hauwezi kuipata. Hii ndio maana tunasimama na kusema kwamba ili tuwe taifa ambalo lina muongozo, Serikali ijaribu kujimudu iwezavyo. Mimi na wenzangu hapa Bungeni, tumefanya siasa kwa miaka mingi, huku tukikemea magendo na rushwa katika Bunge la Kumi. Wengine walikuwa mstari wa mbele nikiwaunga mkono na wakiniunga mkono pia lakini leo hii ninashangaa kiwango cha hali ya magendo katika taifa letu na uporaji wa mali ya umma. Hivi sasa, hata sio kuiba, bali ni “beba twende” ama “ni ngapi, weka kwa kikapu tuondoke”. Bi. Spika wa Muda, leo hii, hakuna nchi ya aibu kama nchi yetu. Tulipokuwa Tanzania kushuhudia kuapishwa kwa Mweshimiwa Magufuli tulishuhudia kwamba magazeti yetu yanasomwa sana katika nchi za kigeni, hasa Afrika Mashariki na kupitia mitandao ambayo ni ya kisasa. Cha kushangaza ni kwamba, ukichukua gazeti la Kenya, kichwa tangulizi cha hilo gazeti ni kuhusu Waziri, Katibu Mkuu ama mukurugenzi ambaye amehusika kwa wizi fulani. Hili siyo tukio la siku moja tu bali ni matukio ya kila siku. Ndiposa hata viongozi wengine wa Afrika wanasema kwamba Kenya ni kama kuna shule ya kufundisha wizi nchini, na unaweza kupata shahada ya wizi katika taifa letu la Kenya. Viongozi wengine wa Afrika wanawambia wananchi wao wasithubutu kuwa kama Wakenya kwa sababu wakiwa hivyo, watakulana mpaka vidole. Sisi tutasimama lini na kusema, imetosha. Hatuendelei mbele na maskini anaendelea kuwa maskini. Bi. Spika wa Muda, ninatabiri na kusema kwamba, hali hii ikiendelea, wale wanaoendesha magari wataanza kufurushwa katika magari kwa sababu mtu ambaye ana shida huwa hajui kutazama yaliyoko mbele yake. Tumbo ikihitaji chakula, mtu huwa hana jambo lingine la kufanya. Kwa hivyo, inafaa tuupitisha Mswada huu wa Sen. Musila mara moja, uende kwa Rais ili aweke sahihi yake na ianze kutkelezwa mara moja. Kama The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}