GET /api/v0.1/hansard/entries/599535/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 599535,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599535/?format=api",
    "text_counter": 322,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kuna yeyote ambaye hafanyi kazi kulingana na sheria, inafaa aseme atafanya kazi katika nchi gani. Nchi yetu sio maskini, kwa sababu ukitembea katika Jiji la Nairobi na uone vile mijengo inaendelea ama ukiangalia magari barabarani, hii ni nchi inajiweza. Wakenya ni watu wanaopenda kufanya kazi. Tunashangaa, kwa mfano, Serikali ya Jubilee inachukuwa Kshs1 bilioni, kuenda kule Galana kufanya miradi ya unyunyizaji maji, na baada ya mwaka moja, tunatangaziwa kwamba Galana Irrigation imetoa gunia 10 ya mahindi baada ya kutumia Kshs1 bilioni. Tunaambiwa kwamba huu ni utafiti unaofanywa. Bi Spika wa Muda, mimi ninashangaa watu wa kutoka Bonde la Ufa, wanasimama na kusema kwamba Serikali inafanya kazi nzuri na huku mahindi ya wakulima maskini wanaotaka kusomesha watoto wao inaoza katika maghala yao. Hii ni nchi au ni pahali pa kuchezea mpira? Hii ni mali ya mtu au ni mali ya Serikali? Hii ni mali ya umma; mali ya maskini wa Wakenya. Kwa hivyo, ukiona jambo kama hilo linafanyika, na sisi tuko hapa tukijigamba kwamba tunaunda sheria, ilhali mambo haya yanapita mbele ya macho yetu. Tunaposema tuko tayari kufa kwa kutetea haki ya Wakenya, tunatishwa na kutupwa jela. Ni afadhali kukaa jela kuliko kukaa nje ukiwa mtumwa. Naunga mkono."
}