GET /api/v0.1/hansard/entries/599568/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 599568,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599568/?format=api",
"text_counter": 355,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kama vile umesema, umenipendelea, nashukuru sana. Nampa pongezi Sen. Musila kwa sababu Mswada huu umebobea kama yeye. Kuna sababu ambazo zinafanya stakabadhi hizi zizuiliwe shuleni. Kuna sababu mpya ambayo imejitokeza. Kuna haya masomo ya ziada ambayo ukienda shuleni kuchukua stakabadhi, utaambiwa hakulipa pesa za remedial . Pia, kuna stakabadhi zingine ambazo zinazuiliwa kwa sababu ya ukosefu wa nidhamu kwa mtoto. Kama mtoto hana nidhamu, na hata kama umelipa karo, utaambiwa zimezuiliwa kwa sababu ya nidhamu. Lazima tuangalie vile tutafanya ama tutawajibika vipi ile watoto wawe na nidhamu. Mwanafunzi ataogopa kwamba stakabadhi yake itazuiliwa kama atakuwa na ukosefu wa nidhamu. Hizi stakabadhi zimetumika hususan wanafunzi wawe na nidhamu kwa kuhofia kuwa hatazipata kama atakosa nidhamu. Sheria hii inafundisha watoto wawe na nidhamu. Inabidi tutafute njia mbadala ya kuwafanya watoto wetu wawe na nidhamu. Ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi. Hizi stakabadhi zimejaa ofisini lakini zinamsaidia nani? Kuna ofisi ambayo inavuja na hizi ni stakabadhi muhimu. Nimefurahi kutokana na Mswada huu kwa sababu Sen. Musila ameeleza kuwa watu wanafaa kupewa stakabadhi na nampa hongera kwa hilo. Hii inamanisha kuwa mkuu wa taarafa ataweza kuamrisha stakabadhi zipewe wenyewe. Sijui hilo litakuwa vipi kwa sababu kuna stakabadhi ambazo zimekaa kwa muda mrefu bila kuchukuliwa na wenyewe. Hii ndio maana hapo awali nilisema kuwa Mswada huu umebobea kama yeye mwenyewe kwa sababu hayo ndio matamanio ya kila mzazi. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Bi. Spika wa Muda, ukizingatia pilkapilka za watoto wanapofanya mtihani, huenda ukajiuliza jinsi jasho lao litafutwa endapo mtu hatapewa stakabadhi yake. Huenda pia mashirika mbalimbali yakalala kwa sababu watoto wetu wengi hawana stakabadhi. Mtu akitafuta kazi, atapatikana hana stakabadhi. Kwa hivyo, kama Serikali ama nchi, hatutajumuika kuangalia jinsi vijana wetu wataishi ama kazi watakazopewa kwa sababu hakuna marefu yasiokuwa na ncha. Wazazi wengi wamekuwa wakilia kuhusiana na swala la karo. Tunataka stakabadhi zitolewe. Mwanafunzi akiingia shuleni muhula wa kwanza ama kidato cha kwanza, inabidi alipiwe karo. Ni bora watoto wetu katika shule The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}