GET /api/v0.1/hansard/entries/599570/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 599570,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/599570/?format=api",
    "text_counter": 357,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "za upili wasiwe wakilipa karo. Iweje mwanafunzi asome Kidato cha kwanza, cha pili, cha tatu na cha nne na asipewe stakabadhi kwa kuwa hakulipa karo hapo mwanzoni? Naibu wa Rais alisema kuwa ada za mitihani zitolewe. Kwa hivyo, tunaelekea pazuri kwa sababu mbeleni, ada zote zitatolewa. Ada hizo zitakapotolewa, basi pia stakabadhi zitafaa kutolewa kirahisi. Nafurahi kutokana na ari na pendekezo la Sen. Musila. Hata hivyo, itabidi Serikali iende mbio zaidi. Wizi wa mitihani umekithiri sana nchini. Iweje mtu apewe stakabadhi ambayo haifanani naye? Iweje mtu ajiunge na chuo kikuu kutumia stakabadhi ambayo haifanani naye? Iweje mtu apewe stakabadhi ambayo majina hayafanani naye? Hali hii imechangia wakuu wa shule kufanya mambo fulani kwa sababu stakabadhi bado ziko mikononi mwao. Huenda wakageuza jina la Sen. Musila na kuandika jina la mtu mwingine kwa sababu Sen. Musila hakulipa karo na pengine hatalipa. Kwa hivyo, kuzuiliwa kwa stakabadhi kumechangia mambo mengi. Bi. Spika wa Muda, kutakuwa na siasa kuhusu swala la kuondoa karo. Sisi ambao hatuna pesa za kulipia watoto karo au stakabadhi za kuruhusu mtoto aende shuleni bila kulipa karo ndio tutakaoumia. Tunaonekana watu duni kwa sababu hatuna uwezo wa kusema mtoto aachwe aendelee na masomo na kwamba karo italipwa wiki ijayo. Kwa hivyo, Mswada huu umenifurahisha sana kwa sababu utatuweka sote kwenye kiti kimoja; bila kuzingatia kuwa wengine wana uwezo wa kulipa karo ama kuongea na walimu. Bi. Spika wa Muda, chura anayejifunza kuongea hulala na kasia. Kwa sababu sisi tunataka tulale na makasia, tunataka sheria itusaidie sote kama Wakenya. Naomba Mswada huu uweze kutekelezwa mara moja. Naunga mkono Mswada huu. Ukiona mti unapurwa sana ama nchi inatajwa sana, jua kuwa ina matunda matamu. Sijui kama Wakenya wanajua hilo. Mara kwa mara, utapata Kenya au Serikali imetajwa. Lazima tuwe pamoja na wenzetu wa upande ule mwingine ili tuone hizi sheria zinapitishwa na kutufaa sisi sote. Sheria ikitungwa katika hili Bunge la Seneti, sio kuwa ati sisi peke yetu ndio tutafaidika au Sen. Musila ambaye yuko upande ule mwingine ndiye atayefaidika peke yake. Bi. Spika wa Muda, mimi ninauunga mkono kwa dhati Mswada huu na ninaufurahia sana kwa sababu baada ya watoto wetu kupitia pilkapilka za mitihani, ni zawadi gani ambayo watapata? Wewe na mimi kama akina mama, tunaelewa kwamba mama anapokuwa mjamzito anatarajia zawadi. Hawa watoto ni kana kwamba wana ujauzito miaka hiyo yote ambapo wanangojea kupata mtoto wa kike au wa kiume, halafu unaambiwa hutapewa ile stakabadhi. Kunguru wanapopigana ni panzi ndio wanafurahia. Ni sawa na mzazi na mwalimu wasiolewana, anayeumia ni yule mtoto kwa sababu hana hatia na hajui kwa nini mzazi wake akose uwezo wa kumlipia karo. Ni zawadi gani ambayo tutawapa watoto wetu? Sheria hii ikiwekwa, itakuwa kama kuwapa zawadi watoto wetu wa shule. Achana na vile vikaratasi vinavyopelekewa watoto shuleni vya kuwatakia kila la heri katika mitihani. Hii ni zawadi kubwa zaidi ya kusema tu:“Utapita.” Je, wajua huyu mtoto karo imelipwa, stakabadhi yake ataipata, mbeleni atatafuta kazi vipi ili afaidike maishani? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}