GET /api/v0.1/hansard/entries/600342/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 600342,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600342/?format=api",
"text_counter": 74,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Ukiangalia maisha ya sasa, vile ambavyo vijana wetu wanavyolelewa na vile wanavyoishi, utakuta kwamba tumepoteza hadhi zetu kama Waafrika na kama Wakenya. Mambo mengi ya kitamaduni tumeyaacha na hii imetuingiza katika matatizo makubwa haswa katika upande wa mavazi na vyakula. Mababu zetu wameishi maisha marefu zaidi kuliko sisi kwa sababu waliegemea vyakula vya kitamaduni na matibabu ya kitamaduni. Mavazi yetu ya kitamaduni tumeyawacha kiwango cha kwamba hata katika Bunge letu, tumeshindwa kujionyesha tumetoka katika asilia gani. Wakati umefika wa Bunge kutenga siku maalum ambayo tunaweza kuvaa kitamaduni ili tuonyeshe vizazi vyetu ni kipi kilicho bora katika utamaduni wetu. Kupitia Mswada huu, tutaweza kulinda mazingira ya utamaduni wetu. Tutaweza kuhifadhi utamaduni wetu kuanzia vyombo ambavyo tulikuwa tukitumia kuanzia vyakula mpaka namna ya kutoa utao kwa watoto wetu. Kwa ushirikiano baina ya Serikali Kuu na serikali za majimbo, tutaweza kuukuza utamaduni wetu ikiwa sote tutazungumza kwa sauti moja na kushirikiana katika kushauriana. Katika maeneo yetu ya Pwani, kuna mavazi ambyo yamepotea. Tulikuwa na hando, vazi ambalo lilivaliwa na akina mama. Mama akivaa vazi hilo, hata akipita, unaona raha anavyotembea. Kuna mavazi ya ushanga ambao tukivaa kiunoni, shingoni na mikononi mpaka miguuni, mama au msichana anapendeza. Leo hii, hayo yote tumeyatupilia mbali na tumeingia katika mavazi yaitwayo tights, ambayo yanaonyesha maumbile ya mwamamke ambayo ni kinyume na dini na utamaduni wetu. Tukiyatilia maanani yale yote ambayo yameandikwa katika huu Mswada, tutaokoa mambo mengi. Kwa upande wa mapishi, vifaa ambayo vilikuwa vikitumiwa na wazee wetu kama vile nyungu na vikaango, chakula ulikuwa ukikila unapata radha tamu ya chakula. Ulikuwa unapata ile radha ya ile mboga. Leo, kutokana na sufuria ambazo tunatumia, saratani ndio hiyo kwa sababu ile sufuria inafikia wakati inaanza kuisha. Haishi kwa sababu imechomeka na moto, ni wewe ambao unakula vile vipande vya ile sufuria. Kwa hivyo, tukihifadhi utamaduni wetu na kuulinda kisheria, tutaweza kuyaokoa maisha yetu pia kulingana na yale ambayo yanatukumba hivi leo. Angalia chombo kinachoitwa uteo. Uteo ni chombo ambacho kimesukwa kupitia mnazi ambacho kinatumiwa na akina mama kudondoa chakula kama vile mchele au maharagwe na kuyatenganisha. Leo, tumekimbilia mambo ya blender na vifaa vingine vya kisasa kinyume na utamaduni wetu. Viko wapi vitu vyetu vya zamani? Hivi ni vitu ambavyo wazungu wanatoka kule wanakotoka kuja kuvifuata na mwisho wanavinunua na wanaenda navyo na sisi tunabaki bila chochote. Wengine hawanunui, wanatumia mbinu zao na wanabeba kwa kisingizio eti ni zawadi lakini akifika kule, hiki ni chombo ambacho kina dhamani kubwa sana. Kwa hivyo, Mswada huu utatusaidia na tutaweza kuwafuatilia wale ambao waliiba utamaduni wetu. Tutadai watulipe kwa kiwango kile ambacho kitakuwa sawa kulingalisha na utamaduni wetu. Ni lazima tuukuze utamaduni wetu na kuulinda. Kule Pwani, mti wa mnazi una mazao na mambo mengi, lakini umewekwa kando. Tukihifadhi yale yanayotokana na mnazi, tutaokoa hata matumizi mabaya yaliyoko leo. Watoto wamepotelea kwa unywaji mbaya wa pombe. Lakini ukiangalia pombe ya mnazi, kwa wale wanayoitumia, ni kilevyo ambacho hakidhuru kama vile pombe za whisky zinavyodhuru. Tukipata njia ya kuhifadhi vitu kama hivyo kwa njia sawa, tutapata manufaa mengi. Kule kwetu, kuna ile changa tunaitumia kama yeast kwa mahamri au mandazi. Pombe ya mnazi ina dhamani zaidi ya vile watu wanavyoifikiria. Iko na mambo mengi sana. Watu wakioza watoto wao, ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}