GET /api/v0.1/hansard/entries/600343/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 600343,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600343/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "lazima kinywaji kile kiweko. Je, leo tunaambiwa tulete makreti ya Tusker . Huo sio utamaduni. Turudini katika utamaduni wetu na tuyavae mavazi yetu ili na sisi tuhesabike katika ulimwengu kuliko vile ilivyo leo. Mpaka hapa ndani ya Bunge ni lazima ujifunge tai na uvae sketi ndio uhesabike kwamba wewe ni Mbunge. Haifai! Tuukuze utamaduni wetu na turudi katika makavadhi yetu. Kupitia Mswada huu, tutaweza kuyalinda yale makaya na kuyakuza mpaka hata watalii wakija, waweze kuyatembelea ili waone utamaduni wetu na wauelewe. Pia, tutakuwa tunawapatia watoto wetu nafasi ya kupata utao na mwongozo kulingana na utamaduni wetu, kinyume na vile ilivyo leo. Watoto wetu wamepotoka kwa sababu ya kufuata tamaduni za kutoka nje. Namshukuru Mheshimiwa ambaye alitayarisha Mswada huu. Tutauunga mkono na kuupitisha haraka iwezekanavyo na tuweke pesa zote hapo kwa sababu tutakuwa tunajiokoa sisi wenyewe."
}