GET /api/v0.1/hansard/entries/600354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 600354,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600354/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Shukrani, Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu. Kwa kweli, utamaduni ni kitu muhimu. Tujiulize utamaduni ni nini? Ni nini kinachangia utamaduni? Hapo ndipo tutafahamu maana ya vile wahenga walivyosema, “Muacha mila ni mtumwa”. Hii inaambatana na msemo unaosema, “Penye wazee hapaharibiki neno”. Ni kwa sababu utamaduni ni mambo ambayo yamechunguzwa na yametokezea kwa muda mrefu, yakahifadhiwa mpaka leo hii na tunayatumia kwa mambo mengine. Hapa nchini, tumetupa utamaduni kidogo. Nakumbuka kwetu Taita Taveta, kulikuwa na utamaduni wa kuhifadhi mazingara. Kulikuwa na mahali wazee walikuwa wanaenda kufanya mazingaombwe yao na kuomba miungu yao. Ikiwa hapakuwa na mvua, baada ya maombi hayo, mvua ingenyesha. Lakini leo hii, hakuna mambo kama hayo na ndiyo maana hakuna mvua kabisa kule kwetu. Vile vile, miti ilikuwa inahifadhiwa. Siku hizi hilo halipo. Misitu yote imeharibiwa na hivi karibuni, itapotea. Nakumbuka tulipokuwa wadogo tukiwa shule za chekechea, tulikuwa tunaongea lugha za kitamaduni. Kuongea peke yake kunachangia pakubwa kuhifadhi utamaduni. Lakini siku hizi, tunapenda kuongea Kiingereza ijapokuwa hatuwezi kuongea kama Mwingereza mwenyewe. Nampa kongole yule ambaye ameleta Mswada huu. Ikiwezekana, sharti Serikali ihifadhi hela za kutosha ili utamaduni ulindwe. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu kwa asilimia mia moja. Ahsante sana, Mhe. Naibu wa Spika."
}