GET /api/v0.1/hansard/entries/600393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 600393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600393/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono Mswada huu. Ninashangaa sana wakati Mheshimiwa mwenzangu anapowambia Wakenya kwamba utamaduni si kitu cha kudumu. Hali katika redio zetu kuna ratiba mbalimbali kama Sulwe FM, Inooro FM na West FM katika nchi ya Kenya. Inamaanisha nini? Lazima turudi nyumbani na tujifunze maadili na utamaduni wa nchi yetu ya Kenya. Hapo awali mama akiwa mjamzito, alikuwa na yale mavazi ya heshima anayovaa. Si kama siku hizi mama anaweza kuwa mjamzito na anavaa suruali ndefu ama kaptula, kuonyesha kwamba sisi tumepoteza utamaduni wetu. Kwa upande wa chakula, tulikuwa na mboga za kienyeji, tulikuwa na mihogo na ndizi. Hivi ni vyakula ambayo vilikuwa vinaleta afya kwa miili yetu. Mhe. Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni alifanya vizuri kuleta Mswada huu kwa sababu tunataka tujikumbushe mahali ambapo tumetoka na pale tunakoenda. Katika upande wa Magharibi tulikuwa na Dini ya Musambwa. Ilikuwa inatuonyesha maadili yetu katika jamii ya Waluhya; jinsi ya kuishi. Lilikuwa ni jambo zuri sana. Licha ya kuwa na makanisa mengi katika nchi yetu ya Kenya, tulikuwa na yale yanatuonyesha sisi kama jamii mahali tutokapo na tuendapo. Ningependa kuwambia wenzangu kwamba utamaduni na maadili katika nchi yetu ya Kenya unaweza kufunza watoto wetu tabia njema. Siku hizi badala ya mtoto kuongea Kiingereza aseme “my father” anasema “buda wangu”. Mambo kama haya yanaturudisha nyuma kwa sababu tutakuwa tunachanganya lugha ambazo haziwezi kufahamika na wananchi wa Kenya, wasomi na wale wanaokuja nyuma yetu. Sisi kama viongozi tunatakikana tuonyeshe mfano mwema. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, iwapo mimi ni kiongozi kutoka jamii fulani, lazima nionyeshe watoto wetu ama watoto wangu utamaduni wa hapo awali kwamba ukipata mtu wa rika yangu, umuite “mama” lakini usimuite bibi yako. Hiyo itatuwezesha sisi viongozi ama wazazi kufunza watoto wetu mila zetu vile zinatakikana. Hapo awali tulikuwa na pombe iliyoitwa busaa . Zamani haungeona mtoto anaketi na wazee na kushiriki unyuaji pombe pamoja. Yeye alikuwa anakaa mbali. Mzee alikuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}