GET /api/v0.1/hansard/entries/600394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 600394,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600394/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "anachukua mrija anapatia mwingine na anatoka nje. Anapeana heshima. Wakati huu ninaona watu rika yetu wanakula na kukaa pamoja na watoto wetu, ama unaona mtoto akirukia kitanda cha baba ama mama yake. Ninaunga mkono tuwe na huu utamaduni ili tujifahamishe mahali ambapo tumetoka. Ninajua Serikali yetu itahakikisha kwamba kuna mahali ambapo tutakuwa tunafanyia utamaduni wetu. Ninashukuru kwa sababu katika Trans-Nzoia County, nimetembelea sehemu ya ndugu yangu Mheshimiwa Fedinard K. Wanyonyi na kuona kwamba jamii tofauti tofauti wametenga siku ya ukumbusho wa tamaduni zao. Wanapika chakula chao cha kitamaduni na kuvaa mavazi kujikumbusha walikotoka. Jambo hili ni bora sana. Mwaka uliopita niliona mama amejifungua mtoto mlemavu lakini hakutaka watu wamuone. Lakini katika maadili na utamaduni wetu, ukijifungua mtoto kama huyo, watu wanasema huenda ikawa ni bahati sio laana katika jamii. Ninaunga mkono Mswada huu ili kuhakikisha tunahifadhi maadili na tamaduni zetu katika nchi ya Kenya. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}