GET /api/v0.1/hansard/entries/600407/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 600407,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600407/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Ninachukua fursa hii kutoa kongole kwa Kiongozi wa Wengi Bungeni kwa kuleta Mswada huu hapa. Mada na maudhui ya Mswada huu ni kulinda mila na desturi yetu kama taifa. Mhe. Kang’ata aliyenitangulia amenisikitisha akisema kuwa mila yetu kama Waafrika haina maana. Ni kwa masikitiko makubwa hayuko na sisi ndani ya hii Bunge. Ningependa kumwambia kwamba watu wamemwaga damu au wamekufa kwa minajili ya kulinda mila ya Mwaafrika hapa Kenya. Anataka kutuambia wale waliopigania Uhuru wa taifa hili walikuwa wajinga? Ningemwambia arudi darasani ajue mila ni nini. Nimebahatika kusoma kitabu kilichoandikwa na Prof. Asmerom Legesse. Prof. Legesse ameandika kitabu kinachoitwa “ Oromo Democracy” . Amezungumza juu ya Wazulu wa South Africa vile wanaweza kufunza jeshi la kitamaduni la Kiafrika waweze kulinda taifa lao. Pia, amezungumza kuhusu utawala wa Buganda na vile ambavyo Mfalme wa Buganda anaweza kutawala nchi ile bila msaada wa wakoloni. Amezungumza kuhusu jamii ya Waoromo ambao wako katika nchi za Ethiopia na Kenya. Wako na taasisi tatu za ajabu: Serikali ya utawala, bunge na mahakama ya desturi iliyokuwepo kabla mkoloni aje. Rais wao anaitwa “Bagada”. Inafurahisha kumpata Mwafrika aliyefika kiwango hicho. Rais wa Oromo anatawala kwa muda wa miaka minne. Baada ya miaka minne, anampatia mtu mwingine mamlaka. Hakuna kuuana au kuzozana. Hiyo ndio mila ya Mwafrika. Ninaomba Mheshimiwa aliyesema kwamba mila ya Kiafrika haina maana akisome kitabu kinachoitwa “ Oromo Democracy” The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}