GET /api/v0.1/hansard/entries/600408/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 600408,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600408/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Tumepata nini kutoka kwa wazungu? Tumepata bunduki na utumwa. Mila ya Kizungu tuliyonayo leo katika nchi ya Kenya ni mila tumelazimishwa tuifuate kwa kutishiwa na bunduki. Ninasikitika kuwa siwezi kuingia katika Bunge hili bila tai. Ni masikitiko makubwa sana. Bunduki walioleta imeenda lakini sheria zao bado ziko. Sikubaliwi kuzungumza Bungeni mpaka nije na tai. Lini Mwafrika atazinduka na kuwa na uhuru? Angalia tulivyopoteza mila. Mwafrika alikuwepo kwa miaka na miaka. Kwa masikitiko makubwa, angalia vile ambavyo ukahaba kiasi cha umalaya ulivyoenea mijini mwetu. Angalia vijana wetu. Kila mmoja wao anatumia madawa ya kulevya kwa sababu tumepoteza maadili kama jamii. Ninasikitika kwamba wengine wanatuambia kuwa Mwafrika hana mila au mila yake haifai. Wanataka kwenda Uzunguni. Nimekuwa Uzunguni. Ukitaka kujua ukosefu wa mila ni nini angalia watoto wa Wazungu. Kuna sheria na polisi. Huwezi kumtuma yule mtoto. Ukimtuma utashtakiwa. Je, huko ndiko Mheshimiwa Kang’ata anataka twende? Hatuwezi kwenda huko. Tuna mila na desturi ambazo lazima ziheshimike. Waafrika walikuwa wanazozana zamani. Kuna tofauti gani kati ya mizozo ya Kiafrika na ya Kizungu? Mwafrika hupigana kwa fimbo au mkuki. Mkuki mmoja hauwezi kuwaua watu kumi. Leo bastola tu inaweza kuwaua nusu ya walio katika Bunge hili. Angalia vita vya Kiafrika, vita vya kimila na maendeleo ya Kizungu. Ikiwa wanaopigana wanakuja na fimbo, mkuki au bunduki ya rashasha, kwa nini mzozo hauishi katika sehemu za Kiafrika? Mzungu amekuja na kutugawanya katika misingi ya kikabila na mikoa. Amesema kuwa mikoa fulani ni bora kwa sababu hapo ndipo alikuwa akilima na kuvuna. Pia amesema kuwa mikoa mingine haina maana. Hiyo ni dhuluma. Leo hii tunavaa tai na tunaendeleza dhuluma ya Wazungu katika nchi yetu. Kwa masikitiko makubwa, wakoloni wametupa makabila 42 humu Kenya. Kuna makabila mengine zaidi ya 40 ambayo hawajatambua. Kwa sababu wakoloni hawakuwatambua na hawakutaka mila au lugha yao, sisi tulipopata utawala huu tuliwaacha katika giza. Jamii za Munywea na Malakote zinaishi Tana River. Ni jamii zilizo na lugha na mila zao. Leo hii hawawezi kuzungumza lugha au kutambua mila yao na hawana desturi kwa sababu wanaitwa “ Other Kenyans ”. Utu na ubinadamu wao umefunikwa na kuchanganywa. Wanaitwa “ Other Kenyans ”. Hawastahili kuwa kabila. Hiyo ni dhuluma. Iwapo tulipigana na kumuondoa mkoloni, ni haki yetu kutambua na kuheshimu mila na makabila ya wanaoishi katika Kenya. Tusianze kuwabagua watu kwa sababu idadi yao ni chache. Hiyo ni dhuluma. Sitachoka kuzungumza juu ya dhuluma mpaka ile siku itaeleweka katika nchi ya Kenya. Ukizingatia taasisi ya ndoa, utafahamu kuwa tumechukua sana mila ya Kizungu mpaka siku hizi kuna mazungumzo kuhusu ushoga na kutooa katika nchi ya Kenya. Tunaelekea wapi? Mwanaume hataki kuoa kwa sababu ataolewa na mwanaume mwingine. Kwa nini? Ni mila tunaridhi kutoka kwa Wazungu kwa sababu tumeendelea sana. Maendeleo haya yanatupeleka wapi? Taasisi ya familia inaporomoshwa. Dunia imefika mahali ambapo ndoa haina maana. Kuoa hakuna maana kwa sababu mwanaume anaolewa. Tunaenda wapi? Ninampongeza Mhe. Duale kwa kuuleta Mswada huu. Nimefurahishwa zaidi na Mswada huu kwa sababu maeneo ya ugatuzi yamepewa wajibu wa kuchangia vipi watahifadhi mila na desturi ya Mwafrika. Kwa hayo machache, ninaomba kuunga mkono Mswada ulioko mbele yetu."
}