GET /api/v0.1/hansard/entries/600560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 600560,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600560/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wetangula",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 210,
"legal_name": "Moses Masika Wetangula",
"slug": "moses-wetangula"
},
"content": " Bi Spika wa Muda, ningependa kumuuliza Mwenyekiti wa Kamati kama anajua ya kwamba Wakenya walemavu wanaoitwa zeruzeru wako katika hatari kubwa ya kutekwa nyara na kusafirishwa hadi nchi jirani, ambapo wanaamini ya kwamba viungo vya miili yao vinaweza kutumiwa kwa ushirikina na uchawi. Namkumbusha kwamba kijana mmoja zeruzeru kutoka Kitale, alitekwa nyara na wahalifu na kupelekwa mpaka nchi jirani ya Tanzania. Aliweza kunusurika wakati polisi walizingira nyumba alimokuwa amewekwa na kuwashika wale wakora na kumrudisha kabla hajajinchwa na mwili wake kukatwakatwa ili viungo vyake vitumiwe kwa uchawi na ushirikina. Je, Serikali inafanya nini ili kutetea na kuwalinda zeruzeru na haki zao kama wananchi na binadamu, ili washirikina na wachawi wasiwe wanawinda, kuwashika na kuwauza ili wachinjwe na viungo vya miili yao vitumiwe kwa mambo hayo ambayo ni kinyume cha sheria na maadili ya kibinadamu?"
}