GET /api/v0.1/hansard/entries/600652/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 600652,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600652/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "akiwa wa kike, basi, hata nguo mpya hatanunuliwa. Hata yule baba hatalipa ada ya hospitali. Kwa hivyo, sisi wenyewe akina mama tunajidhalilisha. Tunawadhalilisha watoto wetu wa kike mpaka hawathaminiwi. Wewe mwenyewe unapomdharau mtoto wako, mtu wa nje hawezi kumthamini. Bw. Spika wa Muda, tumeshuhudia unyanyapaa. Kina mama wanadharauliwa hata kwenye siasa. Sisi tunafanya siasi, ilhali akina baba wanafanya “si hasa.” Kura zitaibiwa ama kampeini zitafanywa usiku. Kama ni mwanamke, ukifika nyumbani kwako baada ya kumi na mbili za jioni, kila mtu atashaanga umetoka wapi. Lakini akina baba hawaulizwi wametoka wapi. Wanaweza kukesha usiku mzima wakifanya kampeni. Atatangamana na akina mama; hatatuulizaa swali lolote. Lakini sisi akina mama hatutakiwi kutafuta kura za akina baba. Ukikaa na kundi la akina baba, utaulizwa ulikuwa na akina nani huko nje. Kwa hivyo, tumenyanyaswa sana kama wanawake katika nchi hii. Tumenyanyaswa kabisa kwa sababu sisi ndio wengi. Itakuwaje hatuna kura? Ninatoka pwani na kuna mama mmoja pekee ambaye alichaguliwa kuwa Mbunge. Kwa hivyo, hiki ni kidonda ndugu ambacho hakina tiba. Hadi pale sisi akina mama tubadilike na tuthamini watoto wetu wa kike. Mtoto wa kike kama hana karo ilhali mtoto wa kiume amepata alama za chini, yeye ndiye atakwend shule kusoma. Mtoto wa kike atatumika pale nyumbani kama kijakazi. Ni uchochole ambao hatujui dawa yake. Nilitamani wale wageni waliokuja waje waongee na nchi nzima. Mila zetu hazithamini kuwa mtu anaweza kupata cheo au kuwa kiongozi mbele ya wanaume. Pia, mila zetu hazituruhusu kuongea mbele ya wanaume. Utaambiwa ujitande, ujifunike ili usionekane sura. Sauti pia utaambiwa ni uchi. Tutaongea saa ngapi kama akina mama, dada zenu au watoto wenu wa kike? Ni maonevu ambayo hatuwezi kuyaeleza. Saa hii kuna mfumo mpya, wanatuambia kile kiti cha akina mama ndicho chetu. Utaambiwa useneta au ugavana ni wa wanaume. Tunyanyaswa sana kama akina mama katika hii nchi yetu."
}