GET /api/v0.1/hansard/entries/600654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 600654,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600654/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, sijataja dini yoyote. Nimetaja mila, kwa hivyo huwezi kujua mimi niko kwa mila gani. Tukitoka hapa nitakueleza. Nilikuwa ninazungumzia itikadi zetu. Mimi kama mwenyeji siruhusiwi kuonekana wala kutoa sauti. Ni unyanyasaji ulioje? Itakuwaje mimi nitafanya kampeni bila kutoa sauti? Huo ndio uonevu ambao Seneta yuaona raha kwa sababu anasema hiyo ni mila yetu. Nasema katika mila yangu, siruhusiwi kuongea mbele ya wanaume au kukaa hadi usiku sana. Sijataja dini ya mtu. Bw. Spika wa Muda, usalama wetu kama akina mama pia ni changamoto. Sijui tukienda kampeni tutavaa nguo gani ili hata sisi tujisitiri. Ile nguo uliyovaa yaweza kupasuliwa au kuraruliwa mbele ya umma. Tunanyanyaswa pia kwa jinsi hiyo kwa sababu hatuna mtu ambaye anatuangalia na kusema: Je, hawa wanalindwa vipi? Tunanyanyaswa pia na wale wanaume kwa sababu sisi ni watu dhalimu. Hatuna mavazi ambayo tutakaa chonjo na sisi pia tujue hapa ngumi ikirushwa, tutajibu namna gani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}