GET /api/v0.1/hansard/entries/600656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 600656,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600656/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nimesema awali wimbo mbaya hauimbiwe mwana. Wakati mwingine tusilaumu Serikali. Ukiangalia hapa ni kama mila zetu sote ni moja kwa sababu hakuna Seneta mwanamke ambaye alichaguliwa. Tunaona katika Bunge hili sote tuko vivi hivi tu; mara leo utaambiwa: “Wewe huwezi kufanyiwa hivi, kupiga kura ya mtu ambaye alikuja hapa na amechaguliwa.” Kwa hivyo, tunanyanyaswa mpaka kwenye Seneti hii. Unyanyasaji uko nyumbani. Bado tunavumilia kwa uchochole ambao tunapata hapa kwa sababu mwenye nguvu mpishe. Yule ambaye amechaguliwa ana nguvu zaidi yako. Kwa hivyo, mimi ninaunga mkono Hoja hii ya Sen. Ongoro. Tujitahadhari kidole na jicho na kilichotuuma jana leo kisitutambae. Asante sana, ninaunga mkono."
}