GET /api/v0.1/hansard/entries/600831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 600831,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/600831/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika. Ninaungana na Waheshimiwa wenzangu kuwakaribisha wageni kutoka Bunge la Kaunti ya Bungoma. Waswahili husema kwamba mgeni hupokelewa mzigo lakini macho huachiwa mwenyewe. Wageni wetu kutoka Bunge la Kaunti ya Bungoma wana macho na kwa hivyo, waone vile tunavyofanya katika Seneti. Pia waone zile wheelbarrow za laki moja ama Ksh40,000. Nawakaribisha wafanyikazi wote kutoka Kwale eneo ambalo ninawakilisha na zile kaunti zingine ambazo wamefika hapa. Hii ndio Seneti na Bunge ambalo linaonyesha kwa hali, mali na vitendo. Asante."
}