GET /api/v0.1/hansard/entries/602108/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 602108,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/602108/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Nakushukuru Mhe. Spika kwa nafasi hii ambayo umenipatia nami niunge mkono ombi ambalo limetolewa na Mhe. Weru. Naomba nichukue nafasi hii kukosoa Kamati ya Kilimo. Tangu tuanze, mmeleta ripoti ngapi hapa Bungeni? Nauliza, Waheshimiwa, hebu tuangalia haya mambo. Mhe. Spika Kamati za Mbunge zimepewa nafasi zijadiliane na ziangalie mambo ambayo yanaletwa kutoka kwa wananchi ili ipate kuyaangaziya na kutoa ripoti Bungeni. Lakini Mhe. Spika nina wasiwasi kwa sababu kuna uzembe ambao hauwezi kukubalika katika Kamati ya Kilimo. Huu uzembe naomba Mhe. Spika, ukomeshwe na hii Kamati. Kama hayo unayosema, tuko na Ripoti katika Kamati ambayo inahusika na mswala ya ratiba ya Bunge na mimi ni mmoja wao. Sijawahi kusoma ripoti zimekamilishwa nikilinganisha hii Kamati ya Kilimo na zingine. Mhe. Spika wako huru kujitetea lakini kuna uzembe wa hali ya juu na lazima huo uzembe ukomeshwe na uishe. Watu ambao wamepatiwa kazi na wanazembea lazima wabadilishwe katika kamati za Bunge. Kama hamtafanya kazi. Mhe. Spika, naomba uchukulie hili jambo kuwa la busara. Kama si hivyo, hii Kamati na wenzake wote naomba uwapatie nafasi wajitetee lakini vile ninavyojua waheshimiwa wenzangu, hebu niambieni ni ripoti ngapi tumesoma kutoka kamati ya Kilimo? Mambo yao ni mengi. Kuna sukari, samaki na leo hii maziwa. Yatakaa siku ngapi kabla hamjaleta ripoti yenu? Naomba Mhe. Spika, wawache uzembe na wafanye kazi."
}