GET /api/v0.1/hansard/entries/602906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 602906,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/602906/?format=api",
"text_counter": 103,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 431,
"legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
"slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, kwa niaba ya mwenzangu, Seneta wa Kaunti ya Kilifi ambaye Ujumbe wao pia uko hapa, ningependa kuwakaribisha. Ningependa waelewe kuwa wao ni jirani zetu na kwamba wakimwona Sen. Madzayo, watakuwa wameniona na wakiniona, basi watakuwa wamemwona Sen. Madzayo. Nilimweleza kwamba mko hapa na akaniomba niwape salamu zake. Aliniomba niwape ujumbe kwamba tuna matarajio makubwa kutoka Bunge zote za kaunti katika kuhakikisha kuwa ugatuzi umeimarishwa. Kwa miaka mingi, sisi Wapwani tumelia kuhusu dhuluma, kutengwa, wizi na uporaji wa rasilmali zetu. Hata hivyo, tumepata fursa ya Serikali za kaunti ili kurekebisha historia ya majanga yaliyotupata. Nawakaribisha katika Seneti ambayo inaenda sambamba na matarajio ya ugatuzi. Tutashirikiana nanyi kwa kila njia kwa sababu Seneti iko tayari kushirikiana na Bunge lolote ambalo litashurutisha serikali za kaunti, wakiwemo magavana na wasimamizi wa serikali zao kuwajibika. Nawakaribisha tena na kuwasihi mpokee salamu za ndugu yangu, Sen. Madzayo, Maseneta kutoka maeneo yote ya Pwani na Meseneta wote wa Taifa la Kenya. Mungu awabariki."
}