GET /api/v0.1/hansard/entries/602960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 602960,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/602960/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mositet",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 608,
"legal_name": "Peter Korinko Mositet",
"slug": "peter-korinko-mositet"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa na Seneta Hargura. Nchi nzima kweli kuna kilio kingi na tumewapoteza watu wengi kwa sababu ya ugonjwa wa saratani. Nimesikiza Seneta Hargura alipokuwa akituelezea zile shida wamepitia katika lile eneo, na vile watu wamepata wasiwasi kiasi kwamba wanataka kuhama maeno hayo. Nilisikia nikiwa na hofu sana rohoni mwangu kwamba Serikali ingeona kwamba eneo fulani lina shida na haijaweza kujitokeza na kuhakikisha wamepeleka wataalamu wa kuangalia na kujua shida ni nini. Bw. Naibu Spika, wakati umefika ambao katika taifa nzima, filimbi ya ugonjwa wa saratani iweze kupigwa na tuweze kushikana ili tuone kwamba ni vizuri tujitolee kwa mbinu zote na tuone kwamba hatutapoteza watu tena. Hata kwa kaunti yangu, ugonjwa wa saratani haukuwa pale mbeleni, lakini siku hizi, kama ni harambee ya wagonjwa hospitali, ni kwa sababu ya saratani. Kama ni maafa, unasikia ni saratani. Kuna shida nyingi hata katika hospitali. Ingekuwa vizuri kama pesa tunazotengea kaunti zingetumiwa kununua vifaa muhimu vya matibabu ili watu wetu wasife kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo. Zaidi ya hayo, uharibifu wa raslimali zetu kama misitu na chemichemi za maji umechangia---"
}