GET /api/v0.1/hansard/entries/602966/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 602966,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/602966/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chelule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi nichangie Hoja hii kuhusu saratani. Sen. Hargura aliongea kuhusu saratani katika kaunti yake na kusema kuwa watu wanataka kuhama kutokana na vifo ambavyo vimetokea kwa sababu ya ugonjwa huo. Ningependa kumjulisha kwamba visa vya saratani viko kila mahali. Ninapoongea, kuna mazishi ambayo yanaendelea katika kijiji changu. Kifo hicho kilitokana na ugonjwa wa saratani. Serikali inafaa kutilia mkazo mambo ya utafiti ili tujue kinachosababisha ugonjwa wa saratani. Tunadhani kwamba ugonjwa wa saratani unasababishwa na mazingira machafu, chakula ama mbolea. Lakini lazima Serikali itenge pesa za kuwezesha utafiti wa kina. Pia, watu wanafaa kuelimishwa kuhusu saratani kupitia vyombo vya habari. Hii ni kwa sababu watu hawaendi kupimwa kama wako na saratani. Watu wengi wanagundua kuwa wana ugonjwa huo wakati wameathirika na wanakaribia kufa."
}