GET /api/v0.1/hansard/entries/603550/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 603550,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/603550/?format=api",
    "text_counter": 181,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumshukuru Mhe. Nyokabi. Hongera. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu unaenda sambamba na Katiba. Kuiwezesha sheria hii kufanya kazi ni lazima tuwe na miumdo mbinu na miundo misingi ya kuwezesha elimu ya uraia iwe ni ya lazima ili Wakenya waweze kuelewa kila kitu na wapate ufahamu. Pia, elimu ya watu wazima ama adult education inafaa iboreshwe ili watu waweze kupata habari na ufahamu. Pia, tukipitisha Mswada huu, tutaweza kufanya maamuzi bora na kushiriki vyema katika miradi ya kitaifa, kuijua miradi ya Serikali Kuu na miradi ya serikali ya ugatuzi. Tutaweza pia kujua majukumu ya serikali ya ugatuzi na huduma ambazo tunafaa kupata kutoka kwa hizi serikali. Tutaweza, pia, kutofautisha miradi iliyofanywa na Serikali Kuu kama vile miradi ya barabara iliyofanywa na Kenya Rural Roads Authority (KeRRA), CDF na ile ambayo imefanywa na serikali ya ugatuzi."
}