GET /api/v0.1/hansard/entries/603649/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 603649,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/603649/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bi. Naibu wa Spika, Wabunge wanatakiwa kuwa katika Ikulu kesho saa kumi jioni. Siku ya Alhamisi, kila Mbunge na kila mwananchi amealikwa ahudhurie ibada ya misa ambayo itaandaliwa na kusomwa na Baba Mtakatifu. Wabunge wamepatiwa mwaliko na vibali vya kuingia. Ninawaomba Wabunge wanisikize kwa makini. Kitu cha kwanza, magari hayatakubaliwa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi. Kwa hivyo, waalikwa watapitia barabara ya Uhuru Highway mpaka karibu na mzunguko wa Museum Hill, na kuacha magari hapo na kuelekea kwa miguu kwenye uwanja. Kwenye lango la kuingia, kutakuwa na wafanyikazi wa Bunge ambao watawaonyesha mahali pa kukaa. Tumeomba tufanye mawili. Kwanza, ile kadi ya mwaliko ambayo umepatiwa imetumwa na askofu Philip Anyolo, ambaye ni Mwenyekiti wa Maaskofu wote Kenya. Ziko hapa sebuleni. Kila Mbunge anaombwa achukue yake. Pili, kila Mbunge ana kitambulisho chake cha kuonyesha kuwa yeye ni Mbunge. Mnaombwa, ili kurahisisha kazi na kwa sababu ya usalama, kila Mbunge abebe kitambulisho chake ili iwe rahisi kwa Wabunge kutambulika ndiyo msije mkasumbuliwa na walinda usalama. Tunaomba hafla hii iwe ya kufana ili kila mtu apate baraka za Baba Mtakatifu. Ninatumai nimejieleza vilivyo. Nitaomba ruhusa nikimaliza tangazo hili niende kwa Ofisi ya Rais kwa sababu kuna tatizo ambalo limetokea kwa wake na mabwana wa Wabunge. Tuliwakilisha majina ya wake na mabwana zetu lakini bado kuna tashwishi ambayo ninaenda kuimaliza. Bila shaka, nitapata wasaa wa kuwasiliana na Wabunge kabla ya muda kuisha."
}