GET /api/v0.1/hansard/entries/603651/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 603651,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/603651/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Misa itaanza saa nne asubuhi siku ya Alhamisi. Mnaombwa, tafadhali, mhakikishe mko hapo mapema maana milango itafungwa ikifika saa tatu kwa sababu za kiusalama. Hatutaki watu kuzungukazunguka wakati ibaada takatifu inaendelea. Ni vyema kila Mbunge achukue nafasi hii ya kipekee kupata baraka za Baba Mtakatifu. Msiichukue kimzaha. Mmeona watu wameanza kuridhiana. Nchi imeanza kupata angalau heri ya kuwa wanaweza kusameheana. Waheshimiwa, chukueni nafasi hii mje nyote. Haijalishi uko dini ipi. Njoni, mmekaribishwa. Ninatumai nimejieleza vya kutosha. Labda kuwe na suala la kufafanua, niko tayari kuwahudumia Wabunge wenzangu. Mungu awabariki. Asante, Mhe. Naibu Spika."
}