GET /api/v0.1/hansard/entries/603909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 603909,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/603909/?format=api",
    "text_counter": 349,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Shukrani, Naibu Spika wa Muda. Nilidhani hunioni, kumbe waniona! Mhe. Naibu Spika wa Muda, mimi nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu anayekuja ni mtu mtukufu, na hata kama dini ni tofauti zote zaelekea kwa Mungu mmoja. Mimi ni Muislamu na najua kwamba Bunge hili lina Waislamu wa kutosha. Nawauliza Waislamu wenzangu, waheshimu Baba Mtakatifu ili tuweze kuhakikisha kwamba tunaenda kukutana na yeye. Baraka hazitoki sehemu moja. Zinatoka sehemu mbalimbali na nina imani kuwa yeye akiwa kiongozi wa ulimwengu, atatupatia baraka zake. Langu tu ni kumuuliza Mwenyezi Mungu, siku moja Baba Mtakatifu aje awe mtu wa Kenya kama Mhe. Gunga, ili tuweze kupata baraka za karibu, kuliko kungoja miaka mingi hadi Baba Mtakatifu Francis aje. Tunataka tuwe na mtu karibu sana. Ingawa Mhe. Gunga anakataa, ni nafasi ambayo angeitumia. Nataka kutoa shukrani zangu za dhati. Itakua si sawa kwetu kusema kuwa tunabaki hapa ilhali kiongozi mkubwa wa dini ya wenzetu anakuja. Nawaomba Wakatoliki wakumbuke kuwa Uprotestanti pia ni dini, na Uislamu pia ni dini. Kiongozi wa Kiislamu pia naye akija siku moja, pia nao wavunje kazi zao na waelekee kumuona ili tuweze kuwa kitu kimoja ndani ya nchi hii. Ahsanteni. Mungu atubariki na naunga mkono."
}