GET /api/v0.1/hansard/entries/604348/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 604348,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/604348/?format=api",
    "text_counter": 60,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Nashukuru sana Mhe. Spika. Ningependa kuunga mkono uamuzi wa Kamati iliyoteuliwa kuleta maridhiano kati ya Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Ni kweli kwamba kumekuwa na matatizo kuhusu makao makuu ya serikali za ugatuzi. Ni muhimu sheria hii ipitishwe ili kuwe na uwazi na uhakika kuhusu mahali ambapo makao makuu yatajengwa. Sehemu zingine kama katika serikali ya Kaunti ya Nyandarua, hatujakuwa na makazi hayo. Tumekuwa tukikodisha ofisi za serikali za Kaunti juu ya maduka. Ni muhimu kuwe na uamuzi wazi kuwa makao makuu ya serikali ya ugatuzi inapatikana mahali fulani. Hii ni kwasababu raslimali zinazotakikana kujenga hayo makao makuu zitumike. Hii itatusaidia kujua kwamba hapa ndipo makao makuu yataendelea kwa muda mrefu na hayatabadilishwa leo au kesho. Pia, naunga mkono sheria hii inayosema kuwa wananchi wenyewe wahusishwe katika uamuzi, iwapo kutakuwa na pendekezo la kuhamisha makao makuu. Naomba serikali iendelee kusaidia zile kaunti ambazo hazina rasilmali namijengo yakutosha ili kuwa na makao makuu ya kaunti. Asante."
}